Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imeanzaa mwaka 2022 kwa maombi Maalum kwa kuliombea TAIFA na  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. 


Maombi hayo Maalum yameandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.  Saitoti Zelothe Stephen Ili kumshukuru Mungu kwapamoja na watumishi wa Halmashauri kwa kuumaliza Mwaka 2021 Salama.


Bw. Saitoti Amemshukuru Mungu kwa kuumaliza Mwaka 2021 salama na amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Taifa na Kumshukuru pia kwa kuiona Handeni kwa jicho la pekee kwa kuiletea fedha kwaajili ya Miradi mbalimbali.


Maombi hayo Maalum yaliongozwa na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Handeni Alhaji Shehe Shaban Mohamed Kizulwa  na Mchungaji Simon Mwakajila ambaye ni Makamu wa Askofu wa kanisa la FPCT Jimbo la Tanga akiwakilisha Jumuiya ya Kikisto. 


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wamemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kujua umuhimu wa kumshukuru Mungu na kuanza mwaka mwingine na Mungu kwa pamoja hivyo wamemuahidi ushirikiano,umoja na kufanya kazi kwa ufanisi.

Share To:

Post A Comment: