Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth amekabidhi vyeti vya usajili na uandikishwaji wa vikundi saba (07) vya wanawake kutoka mitaa tofauti wanaojishughulisha na kugonga kokoto katika Kata ya Kunduchi sambamba na kuwafungulia akaunti za Benki kwa ajili ya kukamilisha zoezi zima la kupata mkopo.


Mh Mahawanga katika ziara yake aliyoifanya tarehe 08/10/2022 kwenye mitaa mbalimbali iliyopo kwenye Kata ya Kunduchi aliguswa sana na wanawake ambao wanapasua kokoto kwa kutumia mikono na kujipatia fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kwa matumizi binafsi hivyo akaona ni vyema kuwapa elimu ya Vikundi, usajili wa vikundi, sambamba na fursa ya mikopo. Hivyo alihakikisha elimu hiyo inaeleweka na kuungana nao kutengeneza Vikundi, kuvisajili na kuungana na Benki ya CRDB kuhakikisha amevifungulia akaunti kupitia Benki hiyo ya CRDB vikundi vyote sita kimoja kikiwa nicha Vijana wenye Ulemavu ambao nao wanafanya shughuli za kugonga kokoto.


Mh. Mahawanga amewaahidi kuwa hatua ya mwisho ameishaitekeleza ambayo ni kuandaa maandiko ya miradi kwa ajili ya Vikundi hivyo ili kupata  mikopo ya asilimia 10% inayotolewa kwenye kila Halmashauri kuhakikisha wanapata mikopo hii ili waweze kujikwamua kiuchumi kama jinsi ilivyo dhamira yake ya kumkomboa Mwanamke wa Dar kiuchumi.


Aidha amewashukuru sana Benki ya CRDB kwa kukubali kujumuika nao kutoka Ofisini na kuja kuwafata akina mama hao ili kuwafungulia akaunti lakini pia amewapongeza wanawake wote waliojitokeza  kwa namna ambavyo wameendelea kushirikiana naye na kusisitiza ataendelea kuwapamoja nao mpaka kuhakikisha lengo kuu la kumkwamua mwanamke kiuchumi linafanikiwa.


Pia amempongeza sana  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kufanya kazi kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amesisitiza kuendelea kumuunga mkono kwa kuhakikisha anatekeleza vyema Ilani ya CCM 2020/25 hasa kwenye suala la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Share To:

Post A Comment: