Na Andrew Chale 


KAMPUNI ya Vodacom kupitia huduma yake ya 'Lipa kwa simu' imetoa punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaolipia malipo yao kwa njia ya mtandao katika mbio za Zanzibar International Marathon zinazotarajiwa kufanyika 18 Julai mwaka huu.


Akizungumza wakati wa uzinduzi mdogo wa utambulisho wa mbio hizo kwa upande wa Tanzania Bara, Afisa Masoko na Mawasiliano, Kitengo cha Lipa Kwa Simu (Vodacom),  Bw. Mario Mpingirwa alisema wametoa punguzo hilo la asimia 10 kwa wateja wao ilikutoa fursa kwa wakimbiaji kujitokeza  kwa wingi kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuchochea Utalii na kukuza uchumi wa bluu visiwani humo.


"Vodacom tumetoa fursa ya kipekee kwa washiriki wa Zanzibar International Marathon wataweza kulipia kwa mtandao kwa kupiga *150*00# au kutumia Mpesa App.


Ambapo kwa kupiga *150*00#, kisha, Chagua lipa kwa M-Pesa alafu Weka namba ya  Lipa ambayo ni 5555660 ikifuatiwa na Weka kiasi "Tanzania shillings", alafu Weka namba yako ya siri ya M-Pesa na baadae...Utapokea ujumbe mfupi (SMS) kuthibisha muamala wako" Alieleza Mario Mpingirwa.

mich

Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika 18 Julai mwaka huu,  kila mshindi ataibuka na zawadi nono:

Zawadi hizo ni pamoja na:  Milioni 3,000,000 (Mil3) kwa washindi wa KM21 kike/kiume, Mil 2,500,000 kwa washindi wa pili na Mil 1,000,000 kwa mshindi wa Tatu huku washindi wengine hadi  10 wataibuka na Tsh Laki moja kila mmoja.


Kwa mbio za KM 10, Mshindi wa kwanza ni Mil 2,500,000, Mshindi wa wa pili  2 ni Mil 1,000,000 na wa Tatu ni Tsh. 750,000.


Mbio za KM 5 mshindi wa kwanza ni mil 1,000,000, wa pili Tsh.750,000 na wa Tatu ni Tsh. 500,000.


Aidha, kwa upande wa Walemavu watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pekee ikiwemo Mshindi wa kwanza ni Mil 1,000,000 wa pili Tsh.750,000 na wa tatu ni 500,000.


"Unaweza kulipia mtandaoni na pia kwa kujiandikisha kupata fomu za ushiriki kwenye maduka ya Dauda sports, Just Fit sports gear Kijitonyama na Mlimani cty na kwa Zanzibar zinapatikana kupitia Cataluna Barbershop iliopo Kiembesamaki, Park Hyatt Zanzibar, Cape Town fish market Zanzibar." Alisema Hassan Mussa Ibrahim msemaji wa mbio hizo.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: