Jane Edward Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Àrusha John Mongela ameihakikishia Kampuni ya Yara kuendelea kutoa  ushirikiano  wa kutosha kwa matumizi ya programu ya Yara Connect unaojihusisha na mbegu za kilimo kwa Mkoa wa Arusha wenye lengo la kusaidia wakulima katika kuweza kutatuliwa changamoto mbalimbali zinazowakabili. 


Akizungumza na wamiliki wa makampuni ya mbegu katika Mkutano ulioandaliwa na Kampuni ya mbegu ya Yara, Mongela amesema kuwa sekta ya Kilimo ni sekta muhimu ambapo wakulima wanaojihusisha na Kilimo hapa Tanzania ni asilimia 58 .


Ameongeza kuwa ,matumizi hayo ya kimtandao yana mchango mkubwa kwenye uchumi wa wakulima hao pamoja na watanzania kwa ujumla kwani watakuwa wakiangalia uwepo wa mbegu mpya katika mtandao na kusaidia kulima kilimo cha kisasa chenye tija.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Yara Tanzania, Burundi na Rwanda Winstone Odhiambo, amesema kuwa lengo ni kuwasaidia wateja kupata mafanikio kupitia matumizi ya mtandao na kuongeza kasi ya utendaji kazi hasa katika sekta ya kilimo.


Ameongeza kuwa, kupitia mtandao huo wauzaji wa mbolea na wakulima wanapaswa kuanza kufikiria kulima kilimo cha kisasa ili kiweze kuwasaidia katika kukuza uchumi.


Kwa upande wao wauzaji wa pembejeo za kilimo, David Mnyamba amesema kuwa programu hiyo itakuwa na faida kubwa kwao na itawezesha wao kuuza bidhaa za Yara kwa kutumia mtandao huo.


Ameongeza kuwa, ili kufikia malengo katika sekta ya kilimo lazima wakulima na wauzaji wa pembejeo kukubali kutoka kutumia matumizi ya analogi na kuhamia digitali ili kuwa na Tanzania yenye usawa.


Hata hivyo uzinduzi huo wa matumizi ya mitandao unatarajiwa kuzinduliwa katika Mikoa saba ambapo wameanzia na Mkoa wa Kilimanjaro na na sasa  Arusha.


Mwisho....

Share To:

Post A Comment: