wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Daudi Mkumbo akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji
kuhusu huduma zao.
wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma
zao
AFISA
Msaidizi wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Mariam Mikidadi akisisitiza
jambo kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga Jiji Tanga wakati wa zoezi la uelimishaji
kuhusu huduma zao.
Msimamizi
wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma
zao
kuhusu huduma zao.
wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma
zao
Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga Jijini Tanga akiuliza swali kwenye mkutano huo
……………………………………………………
 
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) imesema kwamba wanafikiria kuingia kwenye teknolojia ya ufungaji
wa mita za maji ambazo zitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na kuzituma
taarifa kwenye data base ofisini kwao.
Hayo yalisemwa na Afisa Ankra wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Daudi Mkumbo wakati akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya
Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.
Alisema kwani mita hizo zitakuwa
zimefungwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na watu
ambao wanashughulika na usomaji wa mita watakwenda kufanya kazi nyengine
hali ambayo itarahisisha usomaji wake.
“Katika miaka ijayo tunafikiria
kuanzisha mpango huo wa mita hizo lakini zile ambazo tunazotazamia
kuzifunga mwaka huu ni kununua na kufungwa chombo ambacho kinaweza
kupelekea mita kujisoma zenyewe na hao wasomaji waende kufanya kazi
nyengine”Alisema
Afisa Ankra huyo alisema kwamba
anaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja
ambao wanadai kwamba wasomaji hawafiki kwenye maeneo yao kusoma mita.
“Kwa sasa kuna teknolojia ambayo
mtu hataweza kusoma mita ya maji kwa umbali wa mita zaidi ya mita sita
inamaana ndani ya mita sita ndio mtu anaweza kusoma maana yake kila mita
ya maji itakuwa imefungwa kifaa hicho cha GPS ya eneo na ile mita ilipo
atakuwa anatambulika na msomaji akifika ndani ya mita sita hawezi
kudanganya”Alisema
Hata hivyo alishauri wananchi wa
maeneo hayo kuacha tabia ya kutokuacha mabomba wazi wakati wanasubiri
maji yakiwa yamekatika kwani hiyo ndio inaweza kuwa ndio chanzo kikubwa
cha kupata bili kubwa ambayo haihusiani na matumizi ya wateja.
“Kwa sababu kipindi ambacho maji
yamekatika kwenye bomba linajaa upepo hivyo wakati maji yanaporudi
yakiwa na msukumo ule upepe ndio ambao unatangulia kabla ya maji
unaozungusha mita na hiyo ndio chanzo kikubwa”Alisema Afisa Ankra huyo.
Hata hivyo alisema kwamba kama
eneo ambalo ni Duga kuna changamoto ya miuondombinu chakavu aliwashauri
kufunga maji na kutokufungua bomba mpaka wahakikishe maji yanatoka ili
kuepukana na bili kuwa kubwa.
“Lakini ukifungulia maji wakati
hamna maji kwani utasababisha bili kubwa wakati maji yanayorudi huo ni
ushauri mpaka pale ambako yataweza kurekebisha miundombuni ili maji
yaweze kutoka muda wote”Alisema
Hayo yanatokana na malalamiko ya
baadhi ya wananchi kwenye mtaa wa Majengo Kata ya Duga ambao walilamika
kwamba wanapata bili kubwa wakati muda mwengine maji yanakuwa
yamekatika.
Akizungumza mmoja wa wananchi hao
Selemani Rashid alisema kwamba kwenye suala la usomaji wa mita
wanaokwenda kufanya hivyo lazima wakutane na watu waliopo kwenye maeneo
wanayokwenda.
“Lakini muweke utaratibu kwamba
wasomaji wanapokwenda kusoma mita lazima wakutane na watu kwa lengo
kwamba wakati wa usomaji wa mita hizo washughudie namna zinazosomwa ili
kuonda dhana kwamba hawapiti kusoma maji”Alisema
Naye kwa upande wake mkazi
mwengine wa mtaa huo Magreth Jeros alisema kwamba maji yanaweza kukatika
asubuhi mpaka jioni hayatoki na sio siku moja hadi siku mbili lakini
bili zinazokuja zinakuwa ni kubwa sana.
Post A Comment: