Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(kushoto) akipokea vifaa mbalimbali na vyakula kutoka kwa Katibu wa Taasisi ya Neema Foundation Hadija Mwita kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani Hospitali ya Ocen Road
NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaomba wadau mbalimbali waliopo wilaya ya Ilala kusaidia mahitaji kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani waliopo katika hospitali Ocen Road Dar es Salaam.
Sophia Mjema aliyasema hayo leo katika hospitali ya Ocen road wakati wa kupokea vyakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya hospitali hiyo vilivyotolewa na Taasisi ya Wanawake ya Neema Foundation ambapo Mjema alikuwa mgeni rasmi.
Mjema alisema Neema Foundation imejiwekea utaratibu wake kwa mwaka mara moja kusaidia misaada yao pamoja na kushiriki chakula cha mchana na wagonjwa waliopo hospitalini hapo.
"Naomba wadau na Wafanyabiashara kujenga utaratibu wa kusaidia jamii hasa wagonjwa wetu ni sehemu ya kuunga mkono huduma za afya kumuunga mkono Rais wetu John Magufuli kuleta huduma bora za afya karibuni na wananchi "alisema Mjema.
Alisema taasisi hiyo ya Neema Foundation imekuwa kama Wakala imekuwa ikikusanya vyakula na mahitaji mbalimbali kutoka kwa Wanawake tofauti kisha kuviwasilisha kwa ajili ya kusaidia jamii.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais John Magufuli na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanikisha huduma za afya nchi nzima..
Kwa upande wake muuguzi mkuu wa Hospitali ya Ocen road Jecsa Kawegere ameipongeza tasisi hiyo ya Neema Foundation kuwasadia mahitaji ya vyakula amewataka na wadau wengine .
Katibu wa Neema Foundation Hadija Mwita alisema wataendelea kusaidia jamii katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli
Hadija alisema umoja wao una miaka 15 wameweka utaratibu kila mwaka kutoa misaada yao .
Post A Comment: