Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wananchi 600 walioko mtaa wa Burka kata ya Olasiti wanatarajia kupimiwa maeneo yao na kurasimisha ardhi zao iliziweze kutambulika kisheria na pia kuepuka migogoro ya ardhi inayojitokeza mara  mara kwa mara.
Mtendaji wa Mtaa huo Lomitu Loshilu Lukumay  amesema hayo katika mkutano wa Mtaa huo aliowakutanisha wananchi na watalaamu wa upimaji ardhi ambapo amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza hivi punde baada ya kuunda kamati za wananchi ambazo zitaratibu na kusimamia zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi.
Ametoa onyo kali kwa baadhi ya watu wanaoishi kwenye maeneo kwa niaba ya wamiliki kutorasimisha maeneo hayo kwa majina yao na badala yake wamiliki halisi washiriki ili kuepusha migongano .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Upimaji ardhi ya Al.Land Planning Tanzania ltd  Levisy Adriano amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kufanyika kwa kufuata sheria ,kanuni na uadilifu wa hali ya juu lengo na kurasimisha maeneo ya watu wenye kipato cha kati na kipato cha chini kwa gharama nafuu .
Aidha amesema kuwa kwa sasa wananchi wameunda kamati ambazo zitashirikiana na viongozi wa mtaa na kata katika kufanikisha zoezi hilo muhimu.








Share To:

msumbanews

Post A Comment: