Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA anawataarifu wateja na
wakazi wote wa Jiji la Tanga kuwa kutakuwa na kazi ya kusafisha mtambo
wa kuzalisha na kutibu maji ulioko Mowe, siku ya Jumatano, tarehe 19
Juni 2019.
Hivyo, tarehe 19 Juni 2019 hakutakuwa na Maji kabisa
katika jiji kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Baada ya saa 12
joini, baadhi ya maeneo yataanza kupata maji na hali itaendelea
kuimarika kwa awamu.
Hali inategemewa kuiamarika na kurudi kuwa kawaida baada ya siku 5, kuanzia tarehe 20 Juni 2019.
Maeneo yatakayo athirika zaidi Sahare Kisosora, Duga, Masiwani Shamba, Magomeni, Ngamiani na Chumbageni.
Mkurugenzi Mtendaji anawaomba wakazi wa Jiji la Tanga kuhifadhi maji ili wayatumie wakati wa katiko la maji.
Mkurugenzi Mtendaji anawaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0800110111
"Tumia maji kwa Uangalifu,Kila Tone lina Thamani
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Umma
Tanga UWASA
Tarehe 16/06/2019
Kitengo cha Uhusiano na Umma
Tanga UWASA
Tarehe 16/06/2019
Post A Comment: