Home
MIKAKATI
BASHUNGWA ATAJA VIPAUMBELE VYAKE WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent
Bashungwa, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya
kufanya kikao na wakurugenzi wa taasisi 16 na bodi zilizochini ya wizara
hiyo, jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya ushindani
Hamfrey Mosha, akizungumza na wanahabari mda mfupi baada ya kufanya kikao
na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini Dodoma.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usajili wa
biashara na leseni, Emanuel Kakwesi, akizungumza na wanahabari mda mfupi
baada ya kikao cha wakuu wa taasisi na bodi zilizochini ya Wizara hiyo na
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini Dodoma.
Picha na mpiga picha wetu.
..........................
Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.
WAZIRI wa viwanda na biashara Innocent
Bashungwa amezitaka taasisi zilizochini ya wizara hiyo kutengeneza mipango
wezeshi ambayo ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na kutufikisha katika
uchumi wa viwanda, mipango ambayo haitakuwa kandamizi kwa wawekezaji.
Sambamba na kujenga uhusiano mzuri baina ya
taasisi hizo na wenye viwanda, wafanya biashara ili kwa pamoja kuona
changamoto ambazo zinawakabiri wafanyabiashara ambazo ni kikwazo kufikia
malengo.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa
kikao kazi baina ya wakuu wa taasisi kumi na sita (16) pamoja na bodi
zilizochini ya wizara hiyo, waliokutana kwa siku mbili Dodoma kujadili
mbalimbali na namna ya kufikia walengo ya serikali.
Amezitaka taasisi hizo kuja na mbinu ambazo
zitasaidia kuinua sekta hiyo bila kuathiri wawekezaji na kukaa na
wawekezaji kubaini changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika
kutekeleza majukumu yao.
“Lengo la kikao hiki ni kukaa na taasisi
zetu ili kuona namna bora ya kufikia malengo tuliyojiwekea na mambo ambayo
ni kikwazo katika kutekeleza, sasa niwatake taasisi msiwe kikwazo kwa
wawekezaji, mtengeneze mipango ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na
mipango ambayo haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji” amesema Bashungwa.
Ametolea mfano kwa shirika la viwanda
Tanzania TBS kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa kuwa na viwango, pia katika
kudhibiti viwango wahakikishe hawaathiri wala kuchelewesha shughuri za
mwekezaji.
Amesema katika kikao ambacho Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alikaa na wafanyabiashara
ikulu kilimpa mwanga namna ya kuja kufanya kazi ndani ya wizara hiyo na
atahakikisha anasimamia kikamilifu wizara hiyo.
Amesema matokeo ya kikao hicho tayari
yameanza kuonekana ambapo kodi na tozo zilizokuwa kero zimeondolewa zaidi
ya 54, amesema sambamba na hilo atahakikisha anafanya mageuzi katika sekta
hiyo.
Kwa sababu amebaini kuwa unaweza kufuta
kodi hizo lakini tatizo likabaki palepale, amesisitiza kwenye taasisi
kuimarisha mahusiano na wawekezaji na namna ya kuongea na wafanyabiashara,
linaweza kuwa sida sio kero ya kodi bali ni mahusiano baina yao.
Amebainisha kuwa kuna haja ya
kufungamanisha sekta ya kilimo na viwanda ili kuleta matokeo chanya katika
wizara ya viwanda na biashara, amesema kuna uhusiano mkubwa baina ya kilimo
na viwanda hivyo vikifungamanishwa vinaweza leta matokeo mazuri.
Amesema ataimarisha mahusiano na jumuiya
ambazo Tanzania ni mwana chama kama EAC na SADC ili tuweze kufaidika na
kuwa wanachama kwa sababu Tanzania inalipa ada kila mwaka ni lazima ione
matokeo yake na hasa katika sekta ya uwekezaji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya tume
ya ushindani Hamfrey Mosha, amesema kikao hicho kilikuwa na faida kwa
sababu kimezikutanisha taasisi kumi na sita(16) zilizochini ya wizara hiyo
na kujiona kumbe wanaweza kufanya jambo ila walikosa nafasi tu kama
hiyo.
“Kikao kimekuwa kizuri taasisi zaidi ya 16
tumekutana jambo ambalo halijawahi kufanyika na kwa kikao hiki tumejiona
kumbe tunaweza kufanya jambo ndani ya wizara hii” amesema.
Amesema wao kama tume ya ushindani
wanafanya kazi kwa weredi mkubwa kwa kudhibiti bidhaa bandia kuingia nchini
kwa kuhakikisha tunakagua makontena yote yanayoingia katika bandari
zetu.
Back To Top
Post A Comment: