NA HERI SHABAN
JUKWAA la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kata yaKipawa lina idadi ya Wanawake 2000 walojiunga na jukwaa hilo
Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Zipporah Simwanza baadhi yao wameunda vikundi.
Simwanza alisema katika Wanawake 2000 ambao wamejiunga Jukwaa baadhi yao walifanikiwa kuunda vikundi 90 vilivyopo hai vyenye jumla ya Wanawake 1697 ambapo wameungana na kuunda vikundi vya watu watano mpaka hadi 30.
"Kata ya Kipawa ina Jukwaa la Wanawake 2000 Vikundi vikivyosajiliwa 90 wanawake ,1697,vikivyopata mkopo 31.vilivyojaza fomu 19 ambavyo havijaomba mkopo vikundi 40 wasiona vikundi Wanawake 300" alisema Simwanza .
Aidha alisema upatikanaji wa mikopo katika kata hiyo wanawake wengi wanakusudia kukuza mitaji yao wanakata tamaa .
Pia alisema wanakabiliwa na ukosefu wa elimu wameomba halmashauri ya Ilala iwaweze kuwapatia shilingi milioni 40 kugharamia mafunzo ya wajasiriamali zaidi ya 200 kwa kutumia watalaam wa SIDO,TFDA na TBS ili kuwajengea uwezo.
Alisema katika fedha hiyo walioomba itakayobaki watanunua mashine za kukoboa na kusaga pamoja na mashine za kutengeneza mifuko mbadala.
Akielezea changamoto nyingine katika kata ya Kipawa alisema kata hiyo ina mitaa sita,Kipunguni,Stakishari,Mogo,Mji mpya,Kalakata na Uwanja Ndege aina eneo la soko tunaiomba halmashauri iweze kutupatia eneo la soko pindi tunapozalisha bidhaa zetu tujue tunapeleka wapi kata yote aina soko.
Kwa upande wake mgeni rasmi, Katibu wa Jukwaa Mkoa Dar es Saalam Husna
Shechonge aliwapongeza Wanawake wa Kipawa kwa uzinduzi wa Jukwaa hilo watumie nafasi hiyo kuzitangaza fursa za biashara zao na kutafuta masoko.
Husna aliwataka viongozi waliosimikwa katika jukwaa hilo kuwa chachu ya maendeleo katika kushirikiana na wanawake wa kipawa kuakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali kwa lengo la kumkomboa mwanamke kiuchumi .
Husna pia alitoa elimu ya Jukwaa kwa Wanawake alisema Majukwaa ya Wanawake hayana fedha dhumuni lake kutambua nafasi zao walizonazo .
Husna alisema majukwaa ya wanawake yote
ameadhishwa sio kwa ajili ya dhumuni la mikopo majukwaa ya uwezeshaji Wanawake Kiuchumi hayana mikopo
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa Wilaya ya Ilala Sauda Addey amewataka Wanawake kushirikiana kwa pamoja katika shughuli zao za kiuchumi waache maisha tegemezi.
Sauda alisema imefikia Wanawake kujishughulisha wainuke kiuchumi kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano wasiweke chuki katika vikundi waheshimu viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza.
Mwisho
Post A Comment: