Timu ya Taifa ya England imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Croatia kwa idadi ya mabao 2-1.

Katika mchezo huo, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kuamuliwa kuongezwa dakika30 za ziada ili kupata mshindi wa mechi.

England walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 5 ya mchezo kwa njia ya mpira wa adhabu uliopigwa na kuwekwa kimiani na Kieran Trippier na baadaye kipindi cha pili Croatia walisawazisha kupitia kwa Ivan Perisic dakika ya 68.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo, 30 zingine ziliongezwa na Croatia walizitumia vema kwa straika wake, Mario Mandzukic kuandika bao la pili kwenye dakika ya 106.

Mpaka Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo yalibaki kuwa 2 kwa Croatia na 1 kwa England.

Kutokana na England kuondoshwa , sasa itacheza dhidi ya Ubelgiji kusaka mshindi wa tatu Jumamosi huku Croatia ikiungana na Ufaransa kucheza fainali Jumapili ya wiki hii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: