Na Denis Chambi, Tanga.
WAJUMBE wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo, ubora wa kazi pamoja na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.
Katika ziara hiyo, wajumbe wamekagua miradi ikiwemo ujenzi wa Soko la Kisasa la Makorora, ujenzi wa Uwanja Mpya wa Ndege, pamoja na Shule ya Msingi Mbuyuni na Shule ya Sekondari Kasera.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa Duka la Rangi Kange na ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Pongwe, ambayo inalenga kuboresha huduma, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuongeza fursa za wananchi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kusimamia na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia viwango na thamani ya fedha inayotumika, ili iweze kutoa huduma bora na kuchangia maendeleo ya wananchi na Jiji la Tanga kwa ujumla.









Post A Comment: