Na Mwl Udadis Nimejawa na furaha kuona mtu makini ndani ya Jeshi la Polisi mwenye uzoefu na weledi anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuliongoza Jeshi letu la Polisi. Hakika CAMILIUS WAMBURA ni mtu sahihi mno.

Wengi wetu tunaofuatilia utendaji wa Jeshi la Polisi nchini tulitegemea mabadiliko kufanywa hususani katika nafasi hii muhimu ili kupatikana mtu anayeendana na kasi na dira ya serikali ya awamu ya sita.

Baadhi ya nyadhifa na majukumu ndani ya Jeshi la Polisi yaliyowahi kufanywa na IGP CAMILIUS WAMBURA   ni pamoja na;1. Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi - KINONDONI 


2. Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi- Makao Makuu 


3. Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA 


4. Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM 


5. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).


6. Na sasa INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP)


*BAADHI YA SIFA ZA KIPEKEE ZA IGP WAMBURA KATIKA UTUMISHI*


1. Mpenda haki na muwajibikaji


2. Msomi na mwanataaluma mbobezi ndani ya Jeshi la Polisi 


3. Kamanda wa Polisi anayependa kujihusisha na mambo ya kijamii.


4. Mzalendo na mchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi 


5. Kamanda wa Polisi asiye na makuu na mwenye weledi katika nafasi anazo aminiwa.

Pongezi za dhati kwa IGP CAMILIUS WAMBURA, watanzania na hata Makamanda wenzio ndani ya Jeshi la Polisi ni mashuhuda wa uwezo wako na uwajibikaji tunakutakia utendaji mwema.

*************************  MWISHO  ***************************

YOU MAY ALSO WATCH

Matukio ya Kustaajabisha https://youtu.be/yMwpzY2dShc

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: