‎Kariakoo, 9 Octoba, 2026‎

‎Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo, imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Walipakodi kwa kusherehekea pamoja na walipakodi na kuthamini mchango wao katika ulipaji wa kodi. Maadhimisho hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano na kuboresha huduma kwa walipakodi.

‎Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Bw. Severine Mushi, ameipongeza TRA Kariakoo kwa kuvuka malengo na kuitakia utendaji mwema.

Ameahidi kuwa JWK itaendelea kushirikiana na TRA kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari.

‎Aidha, Bw. Severine amesisitiza kuwa Wiki ya Huduma kwa Walipakodi haipaswi kuwa ya maneno pekee, bali ionekane kwa vitendo kupitia huduma bora, kusikiliza changamoto na kutoa majibu kwa wakati, ili kuimarisha utii wa kodi kama ambavyo TRA inafanya kwa sasa.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: