Na Denis Chambi Tanga, 

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga imesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu tangu kuanza kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imeweza kutatua changamoto ya muda wa kuhudumia Meli pamoja na Shehena kutoka simu 20 hadi 5 hali ambayo imepunguza malalamiko ya wadau na wateja wake waliyokuwa nayo hapo awali. 

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Salehe Mbega wakati akiwa katika hafla ya pamoja wateja  na wadau wa Bandari hiyo ikiwa ni muendelezo wa  wiki ya huduma kwa wateja wakiwapongeza kwa namna walivyowezesha  na kuwa sehemu ya mafanikio hayo ambayo yamewezesha utendaji na ufanisi katika kuhudumia upande wa Meli na Shehena na kusaidia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.

"Tulikuwa na changamoto Meli zilikiwa zinasubiri nje kwa muda wa siku kumi hadi ishirini lakini kuhudumia Shehena kwenye Gati ilikuwa ni wastani wa siku 10 mpaka 14 lakini tulikaa na tukafanya tathmini tukiangalia maeneo gani ya kuweza kuboresha tangu uanze mwaka huu wa fedha tumeweza kuwa na wastani mzuri na sasa tunahudumia Meli ndani sikusifuri hadi  tank muda wa kuhudumia Shehena ni ndani ya siku tano pia" amesema 

"Mwaka  ulioisha nilikuwa napokea sana simu za wateja wakiwa wanalalamika  juu ya Meli kuchelewa mizigo yao kutoka ndani ya bandari lakini  tangu tumeanza mwaka mpya wa fedha simu nlizopokea hazizidi tatu maana yake asilimia ya malalamiko ya wateja yameshatatuliwa na  sasa kumekuwa na ufanisi kwenye bandari yetu" ameongeza.

Aidha Menaja huyo amesema kuwa kwa kipindi muda wa mwaka wa fedha uliopita 2025/2026 idadi ya Meli pamoja na Shehena imeweza kuongezeka ambapo kwa upande wa Meli wamevuka lengo la kutoka  meli 360 na kufikia  616 wakati huo huo katika upande wa Shehena ikiwa ni kutoka tani Mil.1,650,000 Hadi tani Mil. 2,179,0000.

"Katika  mwaka wa fedha  uliopita 2025/2026 kwa upande wa Meli tuliweza kuhudumia idadi ya Meli 616 ambapo ilikiwa ni zaidi ya lengo la kuhudumia meli 360, kwa upande wa Shehena iloweza kuongezeka tuliweza kuhudumia tani  Mil.2,179, 000 ambapo lengo lilikuwa ni kuhudumia tani Mil.1,650,000". amesema Mbega.

Amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na wadau na wateja wao ili kuweza kupiga hatua zaidi katika kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.


Wakizungumza katika hafla hiyo baadhi ya wateja wa Bandari hiyo wamepongeza mafanikio ambayo yanaendelea kuonekana hususani baada ya maboresho yaliyofanyika ambapo Meli kubwa zimekuwa zikifika na idadi kuongezeka huku muda wa kuzihudumia ukipungua siku kwa siku.

"Tunawashukuru na kuwapongeza sana Mamlaka ya Bandari  kulikuwa kuna changamoto lakini sasa tunaona zimetatuliwa kulingana na mahitaji ya wakati,  tumeingia Meli zaidi ya mia moja kwa upande wetu sisi Sea front Agent ni ushuhuda tosha" Amesema Amri Meneja wa Sea front Agent.

"Kwa upande wetu sisi tunajivunia sana kwa huduma tunazozipata hapa Bandarini ya Tanga tunajivunia kwa sababu jinsi tunavyopata wateja tunapata ongezeko la ICD nyingine kiujumla huduma ziko vizuri sana" amesema  Meneja wa Chicasa ICD Sophia Mfinaga.




 
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: