NA DENIS CHAMBI, TANGA.


WASHINDI  kupitia maonesho ya  Elimu ujuzi na ubunifu yanayoendelea kufanyika  kitaifa mkoani Tanga  wanatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika maonesho ya kidunia  kwenda kuonesha ujuzi ,ubunifu na maarifa yao.


Hayo yameelezwa na  katibu mtendaji kutoka baraza la Taifa la elimu  ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) Mwajuma Lingwanda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo ambapo amesema jumla ya washiriki 49  waliopatikana kwenye mchujo uliofanyika katika ngazi ya Kanda watashindanishwa  kwenye vipengele 9 ambapo kila  mshidi atakata tiketi ya kwenda kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

"Mashindano haya yalianza katika ngazi ya Kanda ambapo tulikiwa na washiriki  katika maeneo 9 ya ujuzi  na baada ya hapo tumefikia kwenye maonesho ya kitaifa na tuna washiriki 49 kutoka kwenye taasisi mbalimbali waamuzi wako tayari  wale watakaofanikiwa kufaulu na kuwa washindi wa kwanza  watapata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa  mwaka huu"amesema Lingwanda.


Fani hizo zitakazoshindaniwa ni pamoja na mapishi , mekatroniksi, ujenzi, ujuzi wa mitandao,  uchomeleaji wa vyuma , uhandisi, ushonaji wa nguo, na urembo.

Akizungumza Mkurugenzi  mdhibiti ubora kutoka NACTVET Geoffrey Oleke amesema kuwa  ujuzi katika nyanja mbalimbali ni una umuhimu husasani kwa rika la vijana ambao ndio tegemeo na Taifa la kesho hivyo Taifa linapaswa kuwekeza katika elimu ya sayansi.


Amesema mchakato wa kuwapata washiriki wa maonesho hayo ulianza juni 2026 ambapo vyuo vyote vya sayansi vilishiriki katika mchakato katika fani 15 ambapo kati ya hizo  fani 9 zilipata washiriki wengi hivyo kupewa kipaumbele kwa washiriki wa mwaka huu kitaifa ambapo kila fani ina washiriki watano watakaochuana kuonyesha maarifa na ujuzi wao.


"Bila ujuzi kwa Hakika hakuna nchi inaweza ikaendelea kwahiyo na sisi kama nchi tunashiriki kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunakuza ujuzi wa vijana wetu katika shule za sekondari na vyuo ili tupate nguvu kazi iliyo imara ambayo itaisaidia nchi yetu katika kuchochea maendeleo yake" amesema  Oleke.


Maonesho hayo ambayo kwa mwaka huu wa 2026 yamebebwa na kauli mbiu isemayo Elimu ujuzi na ubunifu , njia ya kufikia dira 2050 yameanza kufanyika August 16 yakifunguliwa  rasmi na waziri wa elimu Prof. Adolfu Mkenda huku yakitarajiwa kufungwa August 24 na waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: