NA DENIS CHAMBI, TANGA.


TAASISI za elimu zilizopo hapa nchini zimetakiwa kuendana na  dira ya Taifa ya 2050  katika kupitia masomo tafiti na ujuzi mbalimbali wanaoutoa kwa wanafunzi  wanaosoma ngazi mbalimbali ili kuendana na maendeleo ya teknolojia..


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani wakati alipotembelea na kukagua maandalizi ya maonesho ya wiki ya kitaifa ya Elimu ujuzi na ubunifu yanayoendelea katika viwanja ya shule ya sekondari Usagara ambapo yanayotarajiwa kuzinduliwa rasmi na waziri wa elimu Prof Adolfu Mkenda  17 august 2026.


Dkt.Buriani amesema kuwa Kila taasisi  za elimu Zina wajibu wa kuwaelimisha wananchi juu ya mwelekeo wa kitaifa wa dira ya 2050 ili kutoa ufahamu juu ya malengo ya serikali katika maendeleo  kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo za kielimu.


kaimu mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na masoko kutoka katika chuo cha maji  kilichopo mkoani Dar es salaam chini ya wizara ya maji Godfrey Kituli wakati akizungumza na Msumba Blog katika maonesho ya Elimu , sayansi na ubunifu yanayoendelea kufanyika kitaifa mkoani Tanga ambapo ameeleza kuwa katika kuunga mkono jitihada za serikali juu ya umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji wameweza kupanda miti zaidi ya 1500 katika chuo hicho.


"Kumekuwa na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji  kutokana na shughuli za kibinadamu  tunaendelea kufanya tafiti na kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha vyanzo vya maji  vinalindwa na kutunzwa, tunaiunga mkono moja kwa moja  serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya utunzaji wa mazingira hususani vyanzo vya maji vinavyowazunguka katika maeneo yao". Amesema Kituli.


Maonesho hayo ambayo yanajumuiaha zaidi ya taasisi 300  kwa mwaka 2026 yamebebwa na kauli mbiu isemayo Elimu , ujuzi na ubunifu njia  ya kufikia dira ya 2050 yanatarajiwa kufungwa rasmi august 24 na waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: