Wakala wa Vipimo (WMA) imeungana na wafanyakazi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali nchi nzima kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani.

Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila Mwaka tarehe 1 Mei na kaulimbiu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mwaka 2026 ni *"Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050".

Wakala imeshiriki katika maadhimisho hayo Kitaifa Mkoani Njombe ambapo watumishi wa Mkoa huo wameongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bw. Alban Kihulla.

Pamoja na ushiriki wa Kitaifa kadharika, WMA imeshiriki kuadhimisha siku ya Wafanyakazi katika ngazi za Mikoa kupitia ofisi za Mikoa za Kivipimo.

Uongozi wa WMA unaendelea kuwahimiza watumishi wake kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatoa huduma sahihi kwa wananchi kwa kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo katika sekta mbalimbali.





Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OKULY BLOG

Post A Comment: