NA DENIS CHAMBI, TANGA.


JUMLA ya miradi  ya maendeleo 73 iliyopo mkoani  Tanga yenye thamani  zaidi ya shilingi Bilioni 27.7 inatarajiwa kupitia na mwenge  wa Uhuru kwa mwaka 2026 katika halmashauri 11.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amesema kuwa Mwenge huo  utakimbizwa kwa umbali wa kilomita 1,340  ambapo , miradi 34 itawekewa mawe ya msingi, miradi 26 itafunguliwa na kuzinduliwa, miradi 11  itakaguliwa na baadaye kukabidhiwa mkoani Kilimanjaro junior 28,2026 katika viwanja vya shulen ya msingi Hedalu wilayani Korogwe.


Aidha Balozi Dkt Burian ameongeza kuwa kuwa miradi hiyo ina thamani ya Sh bilioni 27.76, ambapo Sh milioni 300.6 ni nguvu za wananchi, Sh bilioni 1.27 ni michango ya halmashauri, Sh bilioni 10.7 ni fedha za Serikali Kuu huku Shilingi bilioni 15.47 zikiwa ni kutoka katika mchango wa wahisani.


Akizungumzia kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu inayosema,  "Tanzania ni yetu sote tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo amewasisitiza wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kushiriki shughuli zote za Mwenge huo ikiwa ni ishara ya kuonyesha uzarendo kwa Taifa 


"MWENGE huu wa Uhuru ukiwa mkoani Tanga utafanya kazi katika miradi 73 ambapo  utaweka mawe ya msingi jumla ya miradi 34, utafungua na kizindua jumla ya miradi 26 na utatembelea na kukagua jumla ya miradi 11 ya shughuri za vijana na miradi miwili ya maendeleo ya sekta ya maji, miradi hii yote ina jumla ya thamani ya shilingi Bilioni 27,764, 390,480.01." amesema Dkt Burian.


"Fedha ambazo zimetoka katika nguvu za wananchi ni shilingi Million 300,638,449.32, fedha kutoka halmashauri ni shilingi Bilioni 1,79,673,076.72, fedha kutoka serikali ni shilingi Bilioni 10, 707,064,607.76 na fedha kutoka kwa wahisani ni shilingi milioni 15, 477, 014" amebainisha.


Aliongeza kuwa baadhi ya  wananchi watapata fursa ya kuushika na kuukimbiza Mwenge huo kama sehemu ya kuimarisha mshikamano, umoja wa kitaifa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.


Mbali na kuhamasisha maendeleo, Mwenge wa Uhuru utaendelea kutoa elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, malaria, VVU/UKIMWI, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na umuhimu wa lishe bora kwa jamii.


Dk. Burian aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi katika maeneo ya mapokezi, miradi na mikesha mbalimbali ili kushiriki shughuli za Mwenge wa Uhuru na kufaidika na ujumbe wake.


Alisema mkoa umejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanapata burudani na hamasa kupitia ushiriki wa wasanii na vikundi vya sanaa vitakavyoshiriki katika maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utakesha.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: