Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewata wakuu wa Idara mkoani humo kuacha tabia ya kutowapandisha madaraja pindi waongezapo elimu pamoja na kuwazuia kuhama na kwenda kusoma kwani kwa kufanya hivyo ni ishara ya roho mbaya na umasikini.

Mtaka ameyasema hayo alipokuwa wilayani Ludewa mkoani Njombe katika mkutano na watumishi wilayani humo na kuhusisha viongozi wa chama cha mapinduzi na viongozi wa dini.

"Unakuta mtumishi kaenda kujiendeleza kielimu na anastahili kupandishwa daraja halafu mkuu wa Idara unaanza kumzungusha, anataka kuhama unamzuia kwamini umzuie? akihama huyo serikali italeta mwingine atafanya kazi hivyo tuache kujiona tuna mamlaka zaidi ya hadi kuzuia maendeleo ya watumishi wa chini yetu".

Share To:

Post A Comment: