Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka amefanya ziara ya Kimkakati Wilayani Ludewa iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo sambamba na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  amelipa fidia ya Bilioni 15 kwenye mradi mkubwa wa Kitaifa wa Mchuchuma na Liganga ambao upo Wilayani Ludewa

RC Mtaka alipata nafasi ya kutembelea mradi wa Mchuchuma na Liganga haswa katika eneo la Liganga- ambalo ni Tarafa ya Liganga; Kata ya Mundindi ambapo sehemu ya walionufaika na fidia ya Mhe Rais Samia - ni kijiji cha Mundindi ambapo haswa Chuma cha Liganga kilipo.

Kijiji cha Mundindi kimelipwa fidia ya Milioni 400 ambazo fedha hizi uongozi mzima wa Kijiji uliamua kuziwekeza katika Hati Fungani yaani “Bondi” ambazo zinaingizia kijiji faida ya mamilioni ya Fedha ambazo wanazipangia matumizi ya maendeleo wao kama kijiji- Mfano ukarabati wa madarasa, kukata bima kwa wanakijiji wote, kusomesha wahitimu wao Elimu za juu “Scholarship” na mipango mengine mingi inayotekelezeka kwani wana uhakika wa uwepo wa Bajeti toshelezi ya kuwezesha mikakati hiyo kutimia.

Mhe Mtaka amesema hili ni jambo la mfano kitaifa na amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameifanya Wilaya ya Ludewa kuwa Wilaya ya Mfano nchini Tanzania.


Akihitimisha ziara hiyo Mhe Mtaka ametoa pongezi kwa uongozi mzima wa Wilaya ya Ludewa kwa usimamizi mzuri wa fedha ya Serikali iliyotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Mkuu wa Mkoa aliweza kukagua jumla ya miradi ya maendeleo 10 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25 iliyohusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwenye sekta ya Elimu, Afya pamoja na miundombinu ya Barabara na Maji katika ziara hii ya Kimkakati Wilayani Ludewa.

Share To:

Post A Comment: