HOSPITALI ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma kupitia Kitengo cha Kifua Kikuu na Ukoma ,imeanza kampeni maalum ya upimaji wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu  kwa wanafunzi wa shule zote za msingi na sekondari wilayani humo.

Mratibu wa kitengo cha kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dr. Mkasange Kihongole amesema wanafunzi wa bweni watakaokutwa na maambukizi ya TB wataanzishia dawa kama mkakati wa  kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo katika wilaya ya Tunduru

Akizungumza katika kampeni ya uelimishaji,uibuaji na uchunguzi wa ugonjwa huo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kiuma.

“Tunaamini kuwa tunapotoa elimu ya kifua kikuu kwa watoto hasa wanafunzi ni rahisi sana ujumbe kuwafikia watu wengi katika jamii ambao hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na ugonjwa wa TB”,alisisitiza

Amesema ,watoto wanapokuwa likizo wanakuwa kwenye muingiliano na watu mbalimbali na miongoni mwao wapo wanaougua kifua kikuu,hivyo wao kuwa katika hatari ya kupata maambukizi bila kujitambua,na kwamba wanaporudi shuleni ni rahisi kuambukiza wengine.

Amesema kampeni hiyo inafanywa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya kupitia Kitengo cha Kifua kikuu na ukoma kwa kushirikiana na Idara ya Elimu ya Msingi na Sekondari .

Amesema kuwa,katika kampeni hiyo wanafunzi watakaobainika kuwa na maambukizi  ya kifua kikuu watapata matibabu mapema ili wasiambukize wengine .

Serikali imedhamiria kutokomeza ugonjwa ugonjwa wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2030.

Share To:

Post A Comment: