Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka tarehe 22 Machi 2024 amefanya ziara ya kukagua mradi mkubwa wa ujenzi wa  shule mpya ya sekondari inayojulikana kwa jina la Njombe Girls iliyo Wilaya ya Wanging'ombe, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo itakuwa imetumia Bilioni 4 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakati wa Ukaguzi wa shule hiyo Mhe. Mtaka amemtaka Mkandarasi wa Majengo hayo kukamilisha ujenzi wa majengo yote ili kukimbizana ratiba ya masomo ya wanafunzi kwa msimu huu na msimu ujao haswa kwa masomo ya Sayansi.

Aidha Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za uanzishaji na ujenzi wa shule hiyo mpya ya wasichana ya Mkoa wa Njombe.

Share To:

Post A Comment: