Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marryprisca Mahundi amezindua na kukabidhi kisima cha maji kwa wananchi wa kijiji cha Ipumpila, kata ya Ndalambo, wilaya ya Momba, mkoani Songwe ili kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa jimbo la Momba na wilaya yote kwa ujumla wake
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi kisima hicho kwa wananchi wa Ipumpila Ndalambo kupitia maadhimisho ya wiki ya maji Duniani Mhandisi Mahundi amesema pamoja na changamoto ambazo zipo katika baadhi ya maeneo nchini ni dhamira ya serikali kuona maji yanapatikana kupitia Wizara ya maji
Amesema kusudi la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara hiyo ni kuhakikisha maji yanasogezwa hadi kwa wananchi na kwa maeneo ambayo bado hakuna maji safi Wizara hiyo inaendelea kushughulikia kwa mipango ya muda mrefu na muda mfupi ikiwemo kuchimba visima na kuhakikisha jimbo la Momba linafikia wastani wa kitaifa wa upatikanaji wa maji tofauti na ilivyo sasa ambapo Momba ipo chini ya kiwango cha wastani wa upatikanaji wa maji kwa wananchi
Post A Comment: