Mbunge wa Viti Maalumu kutokea mkoa wa Kagera Neema Lugangira ameendelea na  jitihada za kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi na Salama ya kupikia ambapo amezindua awamu ya pili ya kampeni yake ya “Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira” kwa kushirikiana na Shirika la Agri Thamani na Oryx Tanzania ambapo ametoa mitungi 700 kwa Mama Lishe, Walimu, Viongozi wa Dini sambamba na Mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi {CCM}.

Akikabidhi mitungi hiyo ameeleza kuwa anaunga mkono jitihada za Rais Samia ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2032 watanzania wote waweze kutumia nishati safi na salama ya kupikia katika kampeni yake ya “Pika kwa Gesi,Tunza Mazingira” 

Sambamba na hilo Lugangira amekishukuru Chama cha Mapinduzi pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano wanaoendelea kumpatia katika kuwaletea wananchi maendeleo hususani kwenye uzinduzi wa awamu hii ya pili ya kampeni hii,ikumbukwe awamu ya kwanza Mbunge Lugangira aliweza kukabidhi mitungi 300 mwezi september 2023 Bukoba Mjini.

Hata hivyo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Fredy Pallangyo amesema kuwa chama hicho kinampongeza kwa dhati Mbunge Neema Lugangira kwa jitihada zake kubwa za kuendelea kuunga mkono maelekezo ya Rais Dkt Samia na Mwenyekiti wa CCM katika kuchangia utekelezaji wa ilani ya CCM.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi. Fatma Mwasa ambapo aliwaasa wananchi hao waliokabidhiwa gesi kutumia  nishati safi na salama ya kupikia ili kuweza kulinda afya zao kutokana na moshi wanaovuta wakati wa kupika,pamoja na kutunza mazngira na kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kuokoa muda ambao utachangia kuongeza uzalishaji na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Awamu hii ya pili ya Kampeni ya Neema Lugangira ya Pika kwa Gesi,Tunza Mazingira imetekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Agri Thamani sambamba na Kampuni ya ORYX Tanzania.

Share To:

Post A Comment: