1000454585

Ujumbe kutoka Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini na Gesi Asilia nchini Ghana (GHEITI) umefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji jinsi unavyotekelezwa nchini Tanzania katika mnyororo wa maendeleo ya sekta ya Madini.

Hayo yamesemwa leo Disemba 4, 2023 na Mwenyekiti Mwenza wa GHEIT Dkt. Steve Manteaw mapema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Rasilimali Madini ,
Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) katika mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kikazi uliofanyika jijini Dodoma.


Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Manteaw amesema kuwa Tanzania kupitia taasisi ya TEITI imekuwa mfano bora kwa kusimamia shughuli za TEITI kwa kutekeleza vigezo vya Kimataifa kama mpango wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uwazi, Uwajibikaji na Uhamasishaji (EITI) unavyoelekeza kwa nchi wanachama.

1000454574

Dkt. Manteaw amefafanua kuwa jumuiya ya EITI inawachama zaidi ya 57 lakini tumevutiwa na Tanzania ambapo inaonekana kuwa nchi ya mfano mzuri katika uwasilishaji wa ripoti zake ukilinganisha na nchi nyingine ambazo ni wanachama.

Kuhusu mchango wa wachimbaji wa madini nchini , ujumbe huo umevutiwa na mchango wa wachimbaji wadogo kwa kufikia asilimia 40 ya mchango wao ndani ya Sekta hii, huku wakihaidi kuwa wakifika nchini Ghana wataishauri Serikali kuiga mipango shirikishi inayotumika Tanzania ili itekelezwa nchini humo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa TEIT Bw.Ludovick Utouh amesisitiza kuwa pamoja mabadiliko ya kupiga hatua katika Uwajibikaji, Uwazi na Uhamasisha katika usimamizi Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia itaendelea kutengeneza mifumo yake ya ripoti ya kimtandao ili wadau wa sekta husika ndani na nje nchi wapate taarifa za malipo ya kampuni pamoja na mapato ya Serikali kutoka katika kampuni husika.

Utouh ameongeza kuwa kwa kuzingatia kanuni za kimataifa kupitia EITI kwenye sekta ya Uziduaji itazingatia uwazi katika masuala ya mazingira ili kuongeza usimamizi na uwajibikaji wa kimazingira ndani ya sekta hiyo.

Katika mkutano huo Tanzania imewakilishwa na wataalam kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ikiwemo Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini, Ofisi ya Kamishna wa Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ujumbe wa watu kumi na mmoja kutoka taasisi ya GHEITI upo nchini Tanzania kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ndani ya Sekta ya Madini.
1000454581
1000454571
1000454578
1000454576
Share To:

Post A Comment: