Na John Walter-Manyara

Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya Maji na Matope kata nne za wilaya ya Hanang' mkoani Manyara imeongezeka na kufika 65.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema leo imepatikana miili Mingine miwili na kufanya idadi hiyo huku Majeruhi wakiwa ni 116.

Akitoa pole kwa wakazi wa Hanang' leo Mjini Katesh waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema waathirika katika Maafa hayo wanapatiwa huduma zote stahiki na serikali ikiwemo malazi na chakula.

Ameonya watakaotumia misaada hiyo tofauti na lengo, kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Ameelekeza misada yote itakayotolewa na wadau mbalimbali ipitie kwa wakuu wa mikoa kwenye maeneo yao.

Share To:

Post A Comment: