NA:DICKSON BISARE

TIMU ya mchezo wa Darts yaagwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati wakiwa wanajiandaa na safari yao kuelekea nchini Kenya leo katika ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza mbele ya wanahabari mkuu wa msafari wa wachezaji wa timu ya Darts ameongea na kuweza kutoa utaratibu wao kuelekea safari yao.

"Tunafahamu kwamba msafara huu utakuwa wa  kwenda kupambana na takribani nchi tano ambazo zitakuwa ni, Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi.Tunaomba wananchi mtuombee wakati tunajiandaa  na safari hii." Alisema 

Naye,Ndugu Charles  Maguzu Afisa Michezo Balaza la Michezo la Taifa (BMT)  ameanza kuongea kwa niaba ya baraza la michezo na kusema.

"Sisi baraza la michezo la taifa hakika tunawapongeza kwa kazi,na sisi tunawaombea katika kila hatua mnapoenda nchini Kenya katika Michuano yenu.Lakini pia kwa niaba ya watanzania wote ambao wanapenda kushiriki michezo ya Darts waje na kuweza kujifunza jinsi mchezo wa Darts unachezwa." Alisema Charles Maguzu  

Sambamba na hilo ndugu Charles  ameendelea mbele na kuweza kutoa rai yake kwa wazazi waweze kuwatoa watoto wao wasiwabague waweze kuwaleta watoto katika mchezo wa darts.

"Sisi kama baraza la michezo la Taifa (BMT) tunawapongeza kwa hatua hiyo ambayo mmefika, sisi kama baraza tunawahakikishia kwamba tutakuwa pamoja na nyinyi katika hatua zote ambazo mmefikia." Alisema Charles Maguzu Afisa Habari Michezo (BMT) 

Share To:

Post A Comment: