Na Joel Maduka ,Geita


Mke wa askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Biharamulo ambaye amefahamika kwa jina la Monica Zabron (45),amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila tukio ambalo limetokea karibu na kambi ya Burigi Chato sababu zikielezwa kuwa ni msongo wa mawazo uliosababishwa na maradhi ya kansa.


Akizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Sofia Jongo amesema ,Mwanamke huyo ambaye amefikia uwamuzi wa kujinyonga ni mkazi wa Kijiji na Kata ya kasenga Tarafa ya Kachambwa ,Wilayani Chato Mkoani Geita.


Amesema taarifa za awali ambazo zilitolewa na ndugu wa karibu walidai kuwa marehemu amepotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa ameuwawa  lakini baada ya jeshi la polisi kufanya uchunguzi wakishilikiana na jopo la madaktari sita wa Hospital ya Rufaa kanda ya  Chato ndipo alionesha kuwa marehemu alijinyonga mwenyewe sababu zikiwa ni kukabiliwa na msongo wa mawazo ambao umetokana na 

maradhi.


“Tukio lilitokea siku ya tar 9,11,2023 majira ya saa tisa mchana Bi,Monica Zabron alionekana akininginia chini ya Mti akiwa amejinyonga kwa kutumia Kamba ya manila .katika kudhibitisha zaidi mwili ulihamishiwa Hospital ya Chato kwaajili ya uchunguzi na baada ya kuchunguzwa alionekana amejinyonga sababu zikiwa ni msongo wa mawazo ambao umesababishwa na maradhi ya kansa”Sofia Jongo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.


Aidha Kamanda Sofia Jongo ametoa Wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujikatia tamaa pindi wanapokuwa na matatizo na badala yake wakatumia njia Rafiki ya kutatua changamoto zao.


Mwisho..

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: