Na Joel Maduka,Geita 

Mkoa wa Geita umetajwa kuwa ni mkoa wa 7 wenye idadi kubwa ya watu ambao wanaongezeka kila siku hii ikiwa ni takwimu ya Tanzania yote yani bara na visiwani ambapo kuna jumla ya watu milioni 2.9.

 Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Geita  Martin Shigela wakati wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali katika mkoa huo.

Shigela amesema katika sensa ya mwaka 2012 Geita ilitajwa kuwa na watu million 1.7 ukilinganisha na sensa ya mwaka 2022 ambayo inaonesha ongezeko kubwa la watu million 1.2.

"Baada ya miaka 10 tumeongezeka kwa idadi ya watu mil 1.2 sio kwamba tunazaliana sana pamoja na kwamba kule Katoro kila mwezi kuna watoto zaidi ya elf 1000 wanazaliwa lakini chanzo kikuu cha ongezeko la watu ni shughuli za kiuchumi ambazo ndio zimekuwa ni kichocheo kikubwa kwa wananchi kuingia mkoa wa Geita"Martin Shigela Mkuu wa Mkoa wa Geita. 

Kwa upande wake mtakwimu mkuu wa Serikali Khalid Msabaha amesema  kuwa serikali ipo katika utekelezaji wa awamu ya tatu na ya mwisho ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.Ambapo miongoni mwa kazi zinazofanywa ni uchakataji wa taarifa, uandishi wa ripot ,pamoja na usambazaji wa mafunzo na matokeo.

"Hadi  sasa tayari serikari imeshaandaa na kuzindua ripoti 11 za sensa ikiwa pamoja na ya matokeo ya mwanzo ambazo zimejikita katika mgawanyo wa idadi ya watu wa maeneo ya kiutawala hadi ngazi ya kata"Khalid Msabaha Mtakwimu. 

Naye  Mbunge wa Geita mjini Constantine Kanyasu amesema kuwa Geita ni miongoni kwa miji inayokuwa kwa kasi kubwa na kwamba jambo la msingi linalotakiwa ni upangiliaji wa mji ambao utaufanya mkoa huo kuwa kwenye madhari nzuri.

"Mji wetu wa Geita tunajivunia kuwa unakuwa kwa haraka na kuwa na idadi kubwa ya watu niziombe mamlaka zianze kupanga mji  kujua maeneo ambayo tunaweza kuweka Shule ,Zahanati na Barabara"Constantine Kanyasu Mbunge Geita Mjini. 

Mwisho.

 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: