Zaidi ya wananchi 23,000 waishio katika halmashauri ya wilaya ya karagwe,mkoani Kagera na maeneo jirani wataondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za upasuaji, baada ya hospitali ya halmashauri hiyo kuanza kutoa huduma hiyo hii leo. 

Hospitali hiyo iliyoanza kujengwa mwaka 2019 na kukamilika mwaka 2020 ,imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 3.4 huku ikiwa na majengo 14 na watumishi 45.

Bi. Zawadi Jackson ambaye amekuwa mteja wa kwanza kupata huduma hiyo , hospitalini hapo leo,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa huduma hiyo.

“ Kwanza nashukuru nimehudumiwa vizuri sana na mimi pamoja na mwanangu tunaendelea vizuri.Napenda kuishuru sana serikali kwa kutuletea hii huduma hapa kwetu kwani sisi kina mama tulikuwa tunatembea umbali mrefu kufuata hii huduma Bukoba mjini  na sehemu nyingine.Tunaomba tuzidi kuletewa huduma nyingine Zaidi”

Upasuaji huo wa kwanza hospitalini hapo umefanywa na na madaktari Dkt.Karimu Abdalah,Dkt.Mugisha Laurian wakishirikiana Nesi.Irene Mlekio , Nesi.Lydia Kanyinginya huku Bwana Oscar Kilengule akiwa ni mtaalamu wa usingizi.

Share To:

Post A Comment: