Na John Walter-Manyara

Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria askari wa uhifadhi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao katika kutunza uhifadhi na kudhibiti wanyama waharabifu na wakali wanaoingia katika makazi ya Wananchi. 

Kauli hiyo imetolewa na Afisa wanyamapori wa Wilaya ya Babati Christopher Laizer wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wa wanyamapori wa vijiji 10 vinavyounda Jumuia ya Hifadhi ya wanyamapori ya BURUNGE (WMA) Wilayani Babati Mkoani Manyara. 

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo mshauri wa jeshi la akiba wilaya ya Babati Meja Selemani Hango amesisitiza uadilifu katika kazi ili kuendelea kulinda maliasili tulizonazo.

Meneja Mradi wa taasisi ya Chem chem Association  Martin Mng'ongo kupitia Mradi wake wa tuhifadhi Maliasili  unaofadhiliwa na Shirika la watu wa Marekani (USAID) kwa miaka mitatu,  amesema wamelenga kuwawezesha vijana watakaoshiriki kwenye Ulinzi na utunzaji wa Mali asili wakiwemo Wanyamapori kwenye ushoroba wa kwakuchinja kuwa wakakamavu na kutambua maadili ya kazi yao.

Askari mpya wa WMA  anayenufaika na  Mafunzo hayo Ismail Kisiri, amesema kuwa wako timamu kwa kazi ya uhifadhi.

 Ni mafunzo ya ukakamavu ya siku 14 yaliyohusisha askari wapya taktribani 46 kutoka Mamlaka ya Wanyamapori TANZANIA TAWA, Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori BURUNGE -WMA, taasisi ya Chemchem pamoja na halmashauri ya wilaya ya Babati yakilenga kuimarisha usimamizi na udhibiti wa wanyamapori katika Hifadhi ya wanyamapori wa BURUNGE.

Share To:

Post A Comment: