Na John Walter-Babati

Ni mwendelezo wa Maua,  Hivi ndivyo unaweza kusema kwa pongezi zinazondelea kutolewa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusambaza huduma za kijamii kila kona ya nchi zikiwemo za elimu.

Shughuli hiyo imepangwa kufanyika , Septemba 2, 2023 katika ukumbi mpya wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara uliopo jirani na TAKUKURU, ikisimamiwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi  (UWT) mjini Babati.

Katika jambo hilo kubwa litakaloambatana na burudani mbalimbali na elimu juu ya malezi na makuzi, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mjini Babati Eva Luoga amesema kuwa kazi nzuri ya kuwaletea wananchi maendeleo wakiwemo wanawake na watoto katika huduma za afya, zimemsukuma kuandaa kongamano hilo maalum la wazi kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.


Share To:

Post A Comment: