Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

 Kamishna wa jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile amewakumbusha Polisi jamii katika Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, Dini, viongozi wa kimila, wadau pamoja na wananchi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

 Ameyasema hayo kwenye kikao cha Polisi jamii kutoka kwenye kata mbalimbali Mkoani Shinyanga kilichohudhuriwa na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, viongozi wa CCM, viongozi wa Dini, viongozi wa kimila pamoja na viongozi wa kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga.

 Kikao hicho ambacho kililenga kuwajengea uwezo wa pamoja katika jukumu la ulinzi na usalama CP Shilogile pamoja na mambo mengine amewakumbusha kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuzuia na kutokomeza uhalifu Mkoani Shinyanga.

 CP Shilogile ametumia nafasi hiyo kumpongeza kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi kwa kuendelea kushirikiana na viongozi hao hali iliyochangia kupungua kwa matukio ya kihalifu Mkoani humo.

 Amesisitiza kuongeza kasi katika kuzuia na kupunguza au kumaliza kabisa uhalifu ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na Rushwa zinazosababisha migogoro mbalimbali yenye uvunjifu wa amani.

 Kamishna Shilogile ameambatana na mratibu wa dawati la jinsia na watoto ACP- Faidha Suleiman ambaye amewaomba viongozi hao kukemea mmomonyoko wa maadili ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili vinavyoendelea kufanyika katika jamii.

 Naye Kamishna mstaafu WA Jeshi la Polisi Rt Sacp Englibert Kiondo pamoja na mambo mengine amewataka Askari wa kila kata kufuata mila na desturi za jamii husika ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada.

 Baadhi ya viongozi wamelipongeza jeshi la Polisi kwa ushirikiano uliopo huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika hatua mbalimbali za kupambana na uhalifu Mkoani Shinyanga.

 Aidha Polisi wa kata mbalimbali Mkoani Shinyanga wamekiri kupokea maelekezo na ushauri  ambao umetolewa huku wakiwaomba viongozi wa kimila kuendelea kushirikiana katika kutokomeza mila na desturi kandamizi zilizopo kwenye jamii.

 Kamishana wa Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii CP Faustine Shilogile amefanya ziara Mkoani Shinyanga akiwa ameambatana na viongozi wengine kukagua miradi ya Polisi jamii ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo katika jukumu la ulinzi na usalama.

Kamishna wa jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

Kamishna wa jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

Kamishna mstaafu WA Jeshi la Polisi Rt Sacp Englibert Kiondo akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

Mratibu wa dawati la jinsia na watoto ACP- Faidha Suleiman akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.

  

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere awali akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.







Mwenyekiti  idara ya wanawake SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwinjilisti Esther Emmanuel akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: