Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa wito kwa wajasiriamali wote nchini kuchangamkia fursa za maonyesho ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) yanayotarajiwa kufanyika kitaifa October 21,2023 katika mkoa wa Njombe.
Mtaka ametoa wito huo ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa juu ya mkoa huo kuwa mwenyeji wa maonyesho hayo kwa kushirikiana wizara ya viwanda na baishara pamoja na SIDO.
"Tunatarajia maonyesho haya yatakaribisha waonyeshaji katika mnyororo mzima wa nyongeza ya thamani kwenye mazao hususani kwenye teknolojia za kilimo na ufugaji"amesema Mtaka
Mtaka ameongeza kuwa maonyesho hayo yatakaribisha teknolojia mbali mbali ambazo wananchi wa Makundi yote watapata nafasi ya kuona namna ambavyo ulimwengu ulivyokuwa na teknolojia bunifu.
"Wito wangu ni kuwakaribisha wajasiriamali wote Tanzania waweze kufika Njombe na kuchangamkia fursa hii ya maonyesho na tumekuwa na kawaida ya kuwa na maonyesho kwa siku saba lakini tunatamani safari hii yafanyike kwa siku kumi ili kutoa fursa kwa waonyeshaji na hii fursa kubwa kwa wananjombe na mikoa inayotuzunguka"amesema Mtaka.
Post A Comment: