Na Denis Chambi, Tanga
Wanafunzi
 , walimu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu zaidi ya 130 kutoka 
Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga wameshiriki 
kikamilifu katika zoezi la uchangiaji wa damu salama katika hospotal ya 
rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mpya wa 
kiislamu ukiambatana na kukumbuka kifo cha mjukuu wa Mtume (S. A .W) 
Imamu Houssein Ally.
 
Akizungumza
 mara baada ya tukio hilo Mkuu wa shule ya wasichana katika taasisi hiyo
 Sheikh Sajad Hassan amesema kuwa uchangiaji wa damu katika hospitali 
hiyo kawaida yao ya  kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuonesha moyo wa 
kujitolea  wahitaji mbalimbali hususani watoto na mama wajawazito 
waliopo hospital wanaohitaji kuongezewa damu.
"Lengo
 la kuja kuchangia damu hapa hospital ni kujitolea sadaka,  
tunaifungamanisha sadaka yetu na tukio la kuwawa kwa mjukuu wa bwana 
mtume (S.A .W) Hussein Bin Allyy aliyeuwawa mwaka 61 Hijiria huko Irak 
aliyekuwa wakiipigania dini kwa lengo la kukemea mabaya na kuamrisha 
mema,  aliyetoka kutetea wanyonge  na wale waliodhurumiwa" 
"Na
 sisi taasisi ya Al Bilal Muslim hili ni zoezi ambalo  tunalifanya kila 
mwaka tukija kuchangia damu katika maeneo tofauti tofauti lengo na sisi 
ni kuonyesha kwamba tumesimama pamoja na mjukuu wa bwana mtume (S.A.W) 
katika kutetea wanyonge,  damu itasaidia wanyonge,  pia tunasimama na 
kukemea dhuruma zozote  zinazoendelea ulimwenguni" alisema Sheikh 
Hassan.
Kwa upande wake 
mkuu wa  idara ya maabara ya damu katika hospital ya rufaa ya mkoa wa 
Tanga Bombo ,  Sinde Ntobu ameishukuru na kuipongeza  taaisisi hiyo kwa 
kuona  kuwa wanayo nafasi kubwa kuokoa maisha ya watu wanaofika 
hospitalini hapo kupatiwa  huduma ikiwemo kuongezewa damu.
Alisema
 uhitaji wa damu kwa mwezi katika hospital hiyo ni mkubwa tofauti na ile
 inayochangiwa ambapo uhitaji wao  unafikia lita 500 hadi 600 wakiwa na 
upungufu wa damu kwa Unit 250 hadi 300 hivyo kuziomba taasisi na watu 
binafsi kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.
"Tunashukuru 
 sana siku ya leo tupo na wenzetu wa taasisi ya Bilal Muslim ambao kila 
mwaka huwa wanakuja kuchangia damu salama kwaajili ya wagonjwa wenye 
uhitaji wa damu tunawashukuru sana kwasababu kila mwaka wana tukio kama 
hili tunawapongeza kwa moyo wao huo wa kuweka katika kalenda yao" 
alisema Ntobu.
" Sisi 
kama hospital kwa wastani kwa mwezi tunatumia  chupa za damu 500 mpaka 
600 lakini uwezo wa kuchangia damu ambayo inapatikana  mara nyingi  
tunapata unit 250 mpaka 300 kwahiyo uhitaji wa damu kwa wagonjwa ni 
mkubwa ,  kikubwa niiase jamii kwa sababu damu ni huduma ambayo 
hainunuliwi mahali popote bali inatoka kwa wananchi kwenye jamii  
tunahitaji jamii ijitolee damu kwa hiari lakini muamko wa jamii katika 
zoezi hili ni mdogo" alisisitiza.
Mbali
 na uchangiaji wa damu taasisi ya Al Bilal Musilim Mission of Tanzania 
pia iliweza kuchangia vitu mbalimbali ambavyo ni mahitaji kwa wakinamama
 wanaojifungua katika hospital hiyo.
Mkuu wa shule ya wasichana wa taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga ,
 Sheikh Sajad Hassan akishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu salama lililofanyika july 27 katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
 Damu salama iliyokwisha kuchangiwa na walimu , wanafunzi na waumini wa dini ya kiislamu kutoka katika  taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga ,
 Sheikh Sajad Hassan akishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu 
salama lililofanyika july 27 katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga 
Bombo.
 Damu salama iliyokwisha kuchangiwa na walimu , wanafunzi na waumini wa dini ya kiislamu kutoka katika  taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga ,
 Sheikh Sajad Hassan akishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu 
salama lililofanyika july 27 katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga 
Bombo.Baadhi ya vitu mbalimbali ikiwemo sabuni vilivyotolewa kwa wazazi waliopo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayofanywa kila mwaka na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga.






Post A Comment: