Na Denis Chmbi,Tanga.

 MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi "CCM" Mkoa wa Tanga  Rajab Abdurahman amewataka viongozi wa  chama hicho pindi wawapo kwenye majukwaa na mikutano ya hadhara ya kisiasa kujibu hoja za wapinzani kwa njia ya amani busara na upole na sio kutumia matuai kejeli wakizidi kudumisha amani na usalama uliopo hapa nchini.


Rai hiyo ameitoa wakati akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika kata ya Msambweni jijini Tanga ambapo amesema kuwa amani na utulivu vikidumishwa ni nyenzo kubwa ya maendeleo kwa kila mmoja na vikikosekana huleta machafuko kwa taifa ikiwemo mgawanyiko wa matabaka mbalimbali ya kisiasa na  kidini.

"Unapoona amani inaendelea kudumu katika nchi yetu na katika mkoa wetu wa Tanga havijaja kwa bahati mbaya hivi vinakuja kwa mikakati ya maksudi,  tusionyeshe viashiria vya uvunjifu wa amani kwa maneneo na matendo yetu"

"CCM tunayo mengi sana ya kimaendeleo yaliyofanywa na serikali yakuwaeleza wananchi kayika sekta mbalimbali Rais wetu anatumia busara na hekima kuilinda amani  ndani ya nchi yetu lakini wenzetu wanatumia nguvu kubwa kuvunja amani ndani ya nchi yetu" alisema Abdurahman..

Pamoja na hayo mwenyekiti huyo amezindua matawi mawili ya chama hicho ndani ya kata ya Msambweni Vatican City ,Umoja wa wanywa kahawa Mabawaambapo ameagiza mashina na matawi yote yaliyopo ndani ya mkoa wa Tanga kuhakikisha yanatumika kuiunga mkono serikali katika mapambano dhidi ya kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya ndoa za utotoni pamoja na ndoa za jinsia moja.

Akiwa katika shina la Vatican City Mwenyekiyi huyo amesema kuwa "Shina liendelee kutumika katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo,  kusimamia amani na usalama hususan   katika suala la kuiunga mkono serikali katika maswa la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na kupiga vita maswala ya ndoa za jinsia moja".

Aidha ameipongeza serikali kutoa fedha katika kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya kimaendeleo ndani ya  ikiwemo upanuzi wa bandari,  ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani yenye urefu wa  kilomita 50 ambao umegharimu kiasi cha shilingi Billion 67 ambao unaendeleo na ujenzi wa daraja kubwa litakalorahisisha usafiri wa Pangani hadi Bagamoyo pamoja na miradi mingine katika sekta ya elimu,  maji,  afya.

" Sisi watu wa Tanga kwenye miradi ya kimaendelo kutoka january hadi june 2023 tumepewa zaidi ya billion  300  katika ujenzi wa shule, ujenzi wa  miundombinu,  afya, na maji, kuna miradi mikubwa ya kimkakati katika barbara ya Tanga  Pangani hadi Bagamoyo kwa kiwango lami lakini kuna barabara ya kuyoka Handeni mpaka mkoa wa Singida yenye urefu wa Kilomita 384 iliyogharimu  zaidi ya Billion 400" alisema Abdurahman.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman akipandisha bendera ya chama hicho mara baada ya kuzindua tawi jipya la Vatican City lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga , tukio lililoanyika july 26,2023.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman (kulia) akicheza mchezo wa draft mara baada ya kuzindua tawi la Umoja wa wanywa kahawa Mabawa  lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga , tukio lililoanyika july 26,2023.


Share To:

Post A Comment: