Na Magesa Magesa,Arusha

MKUU wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude amewatoa hofu wananchi jijini hapa juu ya uvumi wa  kuwapo kwa maandamano siku ya kupiga kura na kusema kuwa katika Wilaya yake hakutakuwa na maandamano hivyo wananchi wote waliojiandikisha katika daftari la mpiga kura wajitokeze kwenda kupiga kura.

Ameyasema hay oleo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya maandalizi ya uchaguzi na kusema kuwa Serikali kupitia vyombo vyote vya ulinzi na usalama imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hakutakuwa na hali ya uvunjifu wa amani.

“Wananchi msiwe na hofu yeyete ya maandamano siku ya kupiga kura,nawahakikishia Arusha hakutakuwa na maandamano hivyo zipuuzeni taarifa hizo na mjitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura”alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkude alisema kuwa hadi sasa maandalizi kwa ajili ya uchaguzi yanaenda vizuri na kwamba vifaa vyote vya uchaguzi vimekwishawasili na kuhifadhiwa kusubiri siku hiyo na kwamba katika jiji la Arusha lenye mitaa 154 waliojiandikisha kupiga kura ni 4,350,119 na kwamba vituo vya kupigia kura vipo 1051.

Aliwataadharisha wananchi kutoshiriki kujihusisha katika vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani kwani watakaobainika watachukuliwa hatua kali z kisheria na kwamba mara baada ya kuga kura warudi majumbani kwa ajili ya kusubiri matokeo.

“Nisisitize kama mnavyojua jumatano ni siku ya mapumziko, nawasihi wananchi wakishamaliza kupiga kura warudi majumbani kwa ajili ya kusubiri matokeo na wajiepushe na vindo vya uvunjifu wa amani ila kwa yule ambaye ana shughuli zake za kufanya siku hiyo anaruhusiwa  kufanya”alisema Mkude.

Amesema hakuna mwananchi yeyete atakayetembea umbali wa zaidi kilometa tatu kufuata kituo cha kupigia kura kutokana na wingi wa vituo vilivyowekwa hivyo hakutakuwa na kisingizio cha kutokupiga kura kutokana na suala la umbali

Share To:

Post A Comment: