Na Imma Msumba; Arusha 

Wakati Serikali kupitia Mkoa wa Arusha ikiendendelea kukamilisha utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Arusha ulio gharimu gharama ya Shilingi Bilioni 520 hadi hapo utakapokamilika. Ambapo mradi huu ni pamoja na shughuli nyingine umehusisha uchimbaji wa visima virefu 56 na unatarajiwa utakapokamilika na kukabidhiwa utaongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwa zaidi ya asilimia 100 ikiwa ni pamoja na:

Kuongeza kiwango cha kuzalisha maji kutoka wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.Kuongeza idadi ya wakazi wanaopata maji kutoka wastani wa 325,000 hadi kufikia 600,000 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini kila siku.Kupunguza upotevu wa maji kutoka wastani wa asilimia 40 hadi asilimia 25.Kuongeza mtandao wa maji safi kutoka asilimia 44 ya sasa hadi asilimia 100;Kuongeza mtandao wa kukusanya majitaka kutoka asilimia 7.66 hadi asilimia 30

Hali ipo tofauti na matarajio ya walio wengi katika kuelekea kukamilika kwa mradi huu kutokana na wananchi wa Jiji la Arusha kulalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha (AUSWA) kuwapandishia bei ya maji. Juni mosi mwakan huu, Auwsa kupitia mitandao ya kijamii ilitangaza bei mpya za maji kwa makundi ya wateja ambapo majumbani bei kwa Lita 1000 ni sh,1.849 , Taasisi sh,1820 biashara ni sh,2300 viwanda ni sh,3080 viwanda vya vinywaji 3080 na magati ni sh,1000,Hali ambayo wananchi wamelalamika iweje bei za majumbani ziwe juu ilhali maisha ni magumu.

Omary Amiri ni mkazi wa Kiserian Katika kata ya Moshono ambapo anaeleza kuwa tumepata taarifa za kupanda kwa bei yam aji lakini cha kusangaza haya maji yenyewe yanaweza kukaa hata wiki mbili bila hata kutiririka kwenye bomba lake.

“Huku kwetu Moshono bado changamoto ya maji ni kubwa sana,na juzi nimetutaarifu kupanda kwa maji ila bado ukumbuke wanaosoma mita nao kuna muda wanatukadiria hawapiti kabisa angalau kwa sasa hii changamoto naona imeanza kutatulika baada ya kwenda kuripoti maana Ankara ilikuwa inajirudia kwa Zaidi ya miezi kadhaa” Alisema

“Nafahamu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ni mchapakazi sana tunamuomba afike Arusha na ashuke huku chini kuzungumza na sisi wananchi pamoja na viongozi wa mitaa na ili tumueleze hali yam aji ilivyo katika maeneo yetu maana tunateseka sana kwa kweli hususani huku kiserian maji hayatoki kwa wakati.” Aliongezea 

Alisema nakumbuka mwaka jana Rais Samia Suluhu Hassan alivyokuja pale Chekereni kukagua moja ya kile kituo cha kusukumia maji alisema “Mradi umeshaanza kutoa huduma kwenye baadhi ya maeneo na kufikia mwezi Juni, 2022 wananchi wote wa Arusha watakuwa wakipata majisafi na salama” sasa nashangaa kwanini kwenye kata yetu hii na mradi umetupitia kwanini shida yam aji bado ni changamoto mtusaidie na nyie waandishi.

Pia wananchi akiwemo Raymond Mosi na Salma Omour ambao ni wananchi wa Kwamrombo katika Kata ya Muriet walisema pia usomaji wa mita kwaajili ya Ankara za maji nazo pia ni changamoto huku wengine wakibambikiziwa bili kubwa kuliko matumizi halisi na kuiomba Mamlaka husika kuja na njia mbadala ya kulipia kabala ya matumizi kwa ambavyo wanavyofanya Shirika la umeme TANESCO kwa kununua umeme.

Hata hivyo idadi ya wakazi wanaopata huduma za maji imeongezeka kutoka wastani wa watu325,000 hadi kufikia watu 704,860 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini Arusha kila siku.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema malalamiko ya kupanda kwa bei za maji katika Jiji la Arusha kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa) yamewasilishwa Wizara ya Maji ili kuangalia namna bora ya kupunguza bei hiyo au la.

Mongella ametoa ufafanuzi huo ambapo amesema kumekuwa na malalamiko kwa wananchi juu ya upandwaji wa bei za maji huku wananchi wakilalamika kuhusu bei hizo mpya lakini ikimbukwe kuwa (Auwsa) inaendesha mitambo yake kwa gharana kubwa sana.

"Malalamiko tuliyosikia tumewasilisha mamlaka husika na mamlaka husika imeahidi kuja Jijini Arusha kukaa kikao ili kujadili bei ishuke au la kadri watakavyoona inafaa ili wananchi wapate unafuu kwa kiasi gani ila ni kweli bei za maji zimepanda ila si Arusha pekee hata maeneo mengine baadhi bei za maji zimepanda."

Aliongezea kwa kusema kuwa mchakato wa kupanda kwa bei ya maji haijarukwa bali taratibu zote zilifanyika na Auwsa hawajapandisha bei za maji zaidi ya miaka 10 na lazima mjue gharama za uendeshaji mitambo na mafuta zimepanda.

Awali baada ya Auwsa kutangaza kupanda kwa bei mpya za maji kuanzia mwezi huu, malalamiko kwa wananchi yamekuwa mengi huku wengine wakidai upatikanaji wa maji ya uhakika kwenye maeneo mbalimbali ni hafifu huku wengine wakikosa maji hata wiki moja.

Ikumbukwe mradi huu umefadhiliwa na Serikali pamoja na Benki ya Afrika ambopo Serikali ilifanikiwa kupata mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Afrika (AfDB) kwa jumla ya shilingi Bilioni 514 sawa na USD Milioni 233.9 kwaajili ya kuboresha huduma ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru.

Ambapo mradi huu ulizinduliwa na kuwekewea jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi Disemba 02 2018 na Aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Wilayani Arumeru.Share To:

Post A Comment: