WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe , akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Wadau wa Kahawa Juni 23,2023 jijini Dodoma, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 22-23, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) Primus Kimaryo,akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Wadau wa Kahawa Juni 23,2023 jijini Dodoma, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 22-23, 2023.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Wadau wa Kahawa Juni 23,2023 jijini Dodoma, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 22-23, 2023

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Wadau wa Kahawa Juni 23,2023 jijini Dodoma, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 22-23, 2023Na Okuly Julius-Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amewaaigiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwaondoa maafisa kilimo wote waliopo mjini na kuwapeleka vijijini wakafanye kazi kwenye Mashamba.

Bashe, amesema hayo Juni 23,2023 jijini Dodoma alipokuwa akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 13 wa wadau wa kahawa nchini ulifanyika kwa siku mbili.

“Inabidi muwaondoe wote waende vijiji kama ambavyo walivyo walimu leo hii tumegawa pikipiki lakini bado tunaziona mjini hadi wakati mwingine tunatamani hata tuzikusanye zile pikipiki zetu”alisema Bashe 

Ambapo Mhe.Bashe amekiri kuwa ugumu uliopo kwenye mfumo wa kuwafukuza kazi watumishi wa umma kuwa ndiyo chanzo cha wengi wao kufanya kazi kimazoea na kushindwa kuwajibika ipasavyo kuisaidia serikali kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Alisema moja kati ya sababu za serikali kushindwa kufikia azma yake ni watumishi wake kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Hadi umfukuze kazi mtumishi wa umma ni kazi sana kuna mlolongo mrefu sana na mimi sina uwezo huo sijapewa mamlaka hayo ila mimi nitakachofanya kwa mtu yeyote ambaye nitaona anashindwa kutekeleza majukumu yake kuna jengo lipo pale Fifty six nitawapeleka waende kusoma magazeti kama serikali itaendelea kuwalipa mishahara iendele kuwalipa”alisema

Amesema inashanagaza kuona mtumishi wa umma anaingia kazini saa 2:00 asubuhi na kuondoka saa 9:00 alasiri bila kujali kuwa kama amekamilisha kazi zake wakati mkurugenzi wake anakaa ofisi hadi saa 3 usiku.

Kadhalika, ameipongeza Bodi ya Kahawa nchini kwa kufanikisha kuongeza mavuno ya zao la kahawa kwa mwaka hadi kufikia tani 84,000 ikiwa ni kiasi kikubwa kufikiwa tangu Tanzania kupata uhuru.

Alisema ili kuendelea kuimarisha zao la kahawa nchini serikali imepanga kuja na mkakati wa kuhamasisha matukizi ya kahawa ya ndani ili kuwa na uhakika wa soko.

“Nchi ya Ethiopia ambao ndiyo wanaongoza kwa uzalishaji wa zao hili Afrika wao kinachowasaidia pia ni matumizi ya ndani na sisi tunapanga kuhamasisha matumzi ya ndani ili hata soko la nje likiyumba tutaendelea kuwa na uhakika wa kuuza kahawa yetu”alisema

Amesema tayari wameshaandika barua kwa vyuo vikuu 15 na tayari viwili vimejibu na kutoa ruhusa ya kuanzisha migahawa ambayo itakuwa inahamasisha matumizi ya kawaha kwa wanavyuo.

“Kusafirisha kilo moja ya kahawa nje ya nchini ni takribani dola nne lakini kuingiza kilo moja ya kahawa ambayo tayari imeongezwa thamani ni dola takribani 20 hivyo ipo haja ya kuwa na soko la uhakika la ndani kwanza”amesema Bashe

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) Primus Kimaryo, amesema hali ya sekta ya kahawa nchini inazidi kuimarika kila siku kutokana na uwezeshaji mkubwa wanao upata kutoka serikalini  na kwa wadau wa zao hilo.

Amesema kutokana na jitihada zilizowekwa na Bodi hiyo wanatarajia kufikia uzalishaji wa tani 300,000 wa zao hilo katika msimu wa kilimo wa 2025/2026 na kuongeza uzalishaji wa miche milioni 20 ya kahawa kwa mwaka ili kufikia mahitaji ya wakulima.

“Pamoja na kuzalisha miche hiyo milioni 20 kila mwaka pia tunapanga kuboresha huduma za ugani ili kuongozea uzalishaji wa kahawa nchini”amesema Primus

Vile vile, amesema moja kati ya vikwazo vinavyokwamisha ukuaji wa sekta hiyo ni pamoja na matumizi hafifu ya mbolea, miti ya kahawa iliyozeeka, pamoja na mabadiliko tabianchi.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa nchini (TaCRI) Deusdedit Kilambo, amesema ipo kazi ya kufanya ili Tanzania iingie kwenye ushindani na nchi nyingine ndani ya Afrika na nje.

Amesema tafiti zinaonyesha kuwa matumizi hafifu ya mbolea yanachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa mavuno madogo ya kahawa kutokana na udogo unaotumika kulima zao hilo kupungua baadhi ya madini.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: