Bertha Mollel, Arusha

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imesema wataendelea kusogeza huduma za mawasiliano zaidi maeneo ya vijijini ili kuwapa fursa wananchi waishio maeneo hayo kunufaika kiuchumi hasa na shughuli za kitalii za mkoa wa Arusha.

Hayo yamesemwa na meneja wa kampuni ya Vodacom Kanda ya kaskazini George Venanty wakati wa uzinduzi wa duka jipya tawi la Aim mall eneo la Kisongo.

Alisema katika kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma za awasiliano vijijini, wanaanza utekelezaji wa ujenzi wa minara 190 katika maeneo ya vijijini.

"Mbali na ujenzi huo, tunakwenda kuongezea nguvu minara yetu inayotoa teknolojia  ya 2G kwenda 3G na zingine zitakuwa na kasi ya 4G yote kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati muafaka"

Alisema kuwa katika huduma zao wamefanikiwa kuwa na bidhaa mbali mbali hasa rafiki kwa watalii ikiwemo kurahisisha mawasiliano ya kuvuka mipaka lakini pia kufanya mabadiliko ya fedha kimtandao.

"Arusha ni moja ya mkoa wetu wa kimkakati ambao tunawekeza nguvu kubwa kuhakikisha tunasogeza huduma karibu, hasa kutokana na shughuli ya kitalii iliyopo hivyo niwaahidi wakazi wa hapa waendelee kutumia mtandao wa Vodacom ili kunufaika na bidhaa zetu"

Akizindua duka hilo, mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa aliwataka kampuni hiyo kuboresha huduma zaidi za kauli zaidi kwa wateja ili kuweza kuteka soko kubwa la utalii

"Kujali wateja, kauli na mda mfupi wa kutatua tatizo la mteja ni vitu muhimu sana, hivyo hakikisheni huduma zenu zinaegemea zaidi huko ili kuwalinda watalii wanaokuja Arusha kwa wingi wafurahie na kwenda kutusemea mema"

 Aliwataka Vodacom kufungua matawi mengi zaidi ili kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi lakini kupanua wigo wa ajira kwa vijana watakaofanya kazi katika maduka hayo.

Nae Mkurugenzi duka hilo la Vodacom tawi la Aim mall, Davis Rwegasha alisema kuwa watatoa huduma zaidi kwa watalii ambao wamekuwa wakitembelea maeneo hayo kama kituo cha mapumziko na manunuzi wakielekea katika mbugani.

Share To:

Post A Comment: