Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye moja ya majukumu ya kutoa elimu kwa wanachi namna gani ya kuunga mkono miradi inayoletwa na serikali kwenye maeneo 


Na Fredy Mgunda,Nachingwea.


HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea imepokea kiasi cha shilingi millioni 931,500,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya Mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifuzanji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara (BOOST)

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa alisema kuwa wamepokea fedha kiasi cha shilingi millioni 931,500,00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,vyoo na nyumba za walimu.

Kawawa alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa shule ya msingi mpya moja ya Kiegei, nyumba ya 2 in 1 moja katika kata ya Kiegei,ujenzi wa matundu matatu ya vyoo shule ya chimbendenga,shule ya msingi Kaloleni matundu matatu ya vyoo, Mchangani, Namatula,Namkula,Ntila na Tunduru ya Leo wote watajengewa matundu matatu vya vyoo kwa kila shule.

Alisema kuwa kutakuwa na ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Chimbendenga madarasa 6, Kaloleni madarasa 2, Mchangani madarasa 2, Ntila madarasa 2,Namkula madarasa 3, Tunduru ya Leo madarasa 2 na ujenzi wa madarasa ya mfano elimu ya awali katika shule ya msingi Chiwindi.

Aidha mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa aliwaomba wananchi kujitokeza kujitolea nguvu kazi ili kuisaidia kumaliza mradi kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Mhandisi Chionda Kawawa aliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoka fedha katika Halmashauri hiyo kuboresha sekta ya elimu.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: