NA TUMAINI MAFIE, ARUSHA

Vijana  waliohitimu mafunzo ya VETA wametakiwa kutumia Mitandao ya kijamii kupata teknolojia mpya Kila siku Ili waweze kufanya mambo makubwa katika tasnia ya Ufundi.

 Akizungumza katika mahafali ya Vijana waliohitimu Chuo Cha Ufundi VETA Oljoro Mkuu wa mkoa wa Arusha  John Mongela alisema  badala ya kutumia mitandao hiyo kupoteza muda ni vema wakatafuta teknolojia mpya kupitia mitandao hiyo.

 Hata hivyo mafunzo ya ufundi (VETA)ya muda mfupi yaliyofadhiliwa na Shirika la maendeleo la  Ujerumani(GIZ) Kwa kushirikiana na Benki ya KCB Mongela alisema vijana Wana uwezo mkubwa wa kujifunza teknolojia mpya kwenye mitandao ya kijamii.

"Vijana tunatumia muda mwingi sana kwenye simu  mjiulize mnapata nini kwenye hizo simu, tumieni muda mwingi kujifunza ujuzi mpya teknolojia zinaingia Kila siku hivyo kupitia hizi simu za mkononi mnaweza kuwa mafundi wa kisasa zaidi"alisema Mongela.

Alisema mafundi wengi hufanya kazi bila uaminifu hivyo kupelekea kuwepo msemo usemao Fundi wa uhakika ni kinyozi peke yake kutokana na kutofanya kazi Kwa uaminifu .

"Ikitokea umepewa kazi Fanya kama mtaalamu Hadi aliyekupatia kazi aseme Fundi ni huyu siwezi kutumia Fundi mwingine msije mkaendeleza huu usemi wa mtaani kuwa Fundi mzuri ni kinyozi tu"Alisema.

Naye mkuu wa Idara ya masoko,uhusiano na mawasiliano  Benki ya KCB Christina Manyenye alisema katika program hiyo waliandikisha vijana 150 na walifanikiwa kuhitimu vijana 146 katika ufundi wa Mabomba,Ujenzi na  Umeme wa majumbani.

Alisema lengo la programu hiyo ni kuinua uchumi wa watanzania hivyo walitoa nafasi hiyo Kwa vijana wa kitanzania ambapo wamefadhili sehemu Mbalimbali mbali ikiwemo Arusha Zanzibar

Alitoa wito Kwa vijana kutumia Elimu ya ufundi waliyoipata kubadilisha Jamii huku akiwataka kuwa mfano wa kuigwa ambapo alisema  Wanatarajia kufadhili vijana zaidi 5000 kupitia programu hiyo.

"Mpaka Sasa takribani watu 1880 wamenufaika na pragramu hii, lakini tulimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa tutawafadhili vijana zaidi ya 5000 hivyo mwezi wa sita wataingia wengine vyuoni"Alisema Manyenye

Share To:

Post A Comment: