Waziri wa katiba na sheria Dkt.Damas Ndumbaro akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika TLS unaoendelea Jijini Arusha uanoenda sambamba na Uchaguzi wa Chama hicho picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Rais wa Chama Cha Mawakili wa Tanganyika TLS Prof.Edward Hosea akiongea katika mkutano Chama Cha Wanasheria Tanganyika TLS unaoendelea Jijini Arusha uanoenda sambamba na Uchaguzi wa Chama hicho


Na Ahmed Mahmoud

CHAMA cha wanasheria Tanganyika TLS.kimezindua mihuri ya kieletroniki(Wakili Stamp System) kwa lengo la kuondoa mawakili vishoka ambao kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko mengi ya mawakili kutumika vibaya kwa kuzingatia uhakiki TLS ikabuni mhuri ambao utadurusiwa na kupatikana mahakamani aua mahali popote na taarifa zitaingizwa kwenye mtandao.


Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano mkuu wa chama hicho unaoenda sambamba na uchaguzi ulioanza leo jijini arusha  Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya chama hicho Ibrahim Bendera amesema kwamba mihuri hiyo ambayo ina nembo ya Kodi itasaidia mawakili kujua taarifa za wateja wao na taarifa zitaingizwa kwenye mtandao na kuondoa vishoka kwani itathibitika kwa muhuri huo kuwa na udhibiti.

Alisema zipo faida kubwa ambazo zitasaida kuondoa changamoto ya uwepo wa mawakili feki wanaowagongea mihuri wateja huku wakili husika akiwa hajui na kumsababishia matatizo pindi mteja anapofika mahakamani kupata huduma na kushindwa kupata huduma aliohitaji kwa sababu tu ya muhuri wa wakili feki.

"kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko mengi ya mawakili kutumika vibaya kwa kuzingatia uhakiki TLS ikabuni mhuri ambao utadurusiwa na kupatikana mahakamani aua mahali popote na taarifa zitaingizwa kwenye mtandao na kuondoa vishoka kwani itathibitika kama mhuri huo huu ni udhibiti"

Akizindua Mihuri hiyo Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema kuna mambo yanahitajika na chama hicho kuyapa kipaumbele ikiwemo suala zima la kuendana na kauli mbiu ya mkutano huo ikiwemo suala la mihuri na kuwapa kipaumbele  vijana katika suala zima la kuwajengea njia ya maendeleo.

Awali akizindua Mihuri Wakili Saccos pamoja na Mtandao wa uchaguzi Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema mihuri hiyo imekuja wakati muafaka kuondoa changamoto mbalimbali ambazo mawakili wamekuwa wakikumbana nazo na serikali ilikuwa kwenye mkakati wa kuasaidia zoezi hilo.

"Mnapoishauri serikali naomba mkatazame namna nzuri itayoendana na ushauri wenye kujenga taswira nzuri ya kujenga tasnia hii nashukuru ushauri wenu mliotoa tunaufanyiakazi kujenga mashirikiano mazuri baina yenu na serikali ila kuna Jambo la kughushi mihuri hili mlitazame kwa upana wake ili kuondoa malalamiko yaliopo katika jamii" alisema Dkt.Ndumbaro

Alisema kuna mambo yanahitajika chama hicho kuyapa kipaumbele ikiwemo suala zima la kuendana na kauli mbiu ya mkutano huo ikiwemo suala la mihuri na kuwapa kipaumbele  vijana katika suala zima la kuwajengea njia ya maendeleo.

Kwa upande wake Rais wa chama cha mawakili wa Tanganyika TLS Prof.Edward Hosea amesema kwa muda mrefu sasa tasnia yetu imekuwa ikiathirika na watu wasio rasmi ambao wamekuwa wakipoteza mapato yetu ndio maana tumekuja na mihuri itakayosaidia watu wasio na sifa kuweza kutambuliwa na kuchuliwa hatua.

"Katika mkutano wetu huo utaambatana na suala zima la uchaguzi ambao kampeni zimeanza tokea miezi miwili iliyopita na kesho itakuwa kwa wagombea kujieleza mbele ya wanachama ambapo kesho kutwa ndio siku ya uchaguzi na kutangaza matokea hii ndio shughuli zetu tunazofanya kila mwaka"alisema Prof.Hosea

Katika mkutano huo TLS imezindua pia Wakili Saccos pamoja na mfumo wa uchaguzi kwa njia ya kieletroniki ambao utaanza kazi mwaka ujao sambamba na mkutano huo kufanya semina kwa wanachama wake tokea mwanzoni mwa wiki hii.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: