Msimamizi wa Mradi wa uendelezaji wa Miundombinu ya Maji Safi Mhandisi Violet Kazumba akitoa maelezo kwa kiongozi wa mbio za mwengi mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma alipotembelea ikiwemo kushiriki kuwaunganishia huduma ya maji safi wakazi wa Kata ya Maweni wawili ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa maunganisho ya maji safi kwa mradi huo

 

Msimamizi wa Mradi wa uendelezaji wa Miundombinu ya Maji Safi Mhandisi Violet Kazumba akitoa maelezo kwa kiongozi wa mbio za mwengi mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma alipotembelea ikiwemo kushiriki kuwaunganishia huduma ya maji safi wakazi wa Kata ya Maweni wawili ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa maunganisho ya maji safi kwa mradi huo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima kulia akipokea mwenge wa Uhuru 2020 leo
Kiongozi wa mbio za mwengi mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma akikagua mradi huo

kiongozi wa mbio za mwengi mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma akikawa mikono mara baada ya kufanya kazi ya ukaguzi wa mradi huo



NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wanawapatia maji safi wananchi na hivyo kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.

Geraruma aliyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa uendelezaji wa Miundombinu ya Maji Safi ikiwemo kushiriki kuwaunganishia huduma ya maji safi wakazi wa Kata ya Maweni wawili ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa maunganisho ya maji safi kwa mradi huo.

Alisema kwamba wametembelea mradi huo na kuona namna mamlaka hiyo ilivyofanya kazi nzuri kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao ya kila siku.

“Kwa kweli niwapongeze Tanga Uwasa kwa kazi nzuri mnayoifanya kuhakikisha mnapaelekea wananchi maji hivyo hakikisheni wananchi wanapolipia huduma hiyo wanaipata kwa wakati ”Alisema

Kiongozi huyo aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha wanafikisha maji kwa haraka kwa wananchi ikiwemo kutekeleza majukumu yao kwa wakati pamoja na wananchi wanapolipia waweze kuunganishiwa kwa muda muafaka ili kuepusha malalamiko yasiyokuwa na tija.

“Ndugu zangu watumishi kama wakati mwengine kuna changamoto muwe mnawaeleza wananchi badala ya kusubiri mpaka walalamike na kuilaumu serikali hii “Alisema Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge.

Hata hivyo aliwakumbusha wananchi kuhakikisha wanajiandaa na kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwani ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi Violet Kazumba alisema kwamba mamlaka hiyo inatekeleza mradi wa uendelezaji wa miundombinu ya maji safi katika Jiji la Tanga kupitia Fedha za Uviko zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19.

Mhandisi Violet alisema mamlaka hiyo imeweza kusimammia mradi wa uendelezaji wa miundombinu ya majai safi Tanga unaogharimu kiasi cha Sh.512,832,602.80 hadi kukamilika wenye urefu wa kilomita 17,640 katika maeneo ya MSD (Mita 4,000),Kichangani-Mji Mwema (Mita 5,125) Mwahako Neema (Mita 3,000),Masiwani Mbugani (Mita 3,300) na Pongwe kusini (Mita 2,215).

Aidha alisema katika utekelezaji wa mradi huo ulioanza Novemba 2021 na kukamilika Mei 17,2022 ambapo kazi zilizofanyika katika mradi huo ni pamoja na upanuzi na ununuzi wa mabomba ya urefu wa mita 17,640,Ujenzi wa Chemba 46 na usimikaji wa alama 353 za kuonesha miundombinu ya maji ambapo kazi zote zimekamilika kwa asilimia 100 na fedha iliyolipwa ni Sh.Milioni 468,366,302 sawa na asilimia 84.



Mradi huo umekusudiwa kuunganisha matawi ya wateja wapatao 1,200 ambapo jumla ya wakazi 7,200 watanufaika na hadi sasa wateja 15 wameshaunganishwa kwenye mtandao wa maji na wameshaanza kupata huduma ya maji safi na salama majumbani mwao.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: