

Na Fredy Mgunda,Iringa
JUMLA ya bilioni 2,169,161,640 zimetumika katika ujenzi na kukarabati barabara
za wilaya ya Iringa zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA) kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa lengo la kuwarahisishia wananchi
usafi na kusafirisha mizigo ambayo inasaidia kukuza uchumi.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya barabara wilaya ya Iringa,meneja wa
TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnaba Jabiry alisema kuwa barabara hizo
zimejengwa kwa kutumia fedha ya tozo za mafuta.
Eng Jabiry alisema kuwa fedha hizo za tozo zimetolewa na serikali kwa lengo la
kuwarahisishia wananchi usafi ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi kwa
wakati na kupata maendeleo yanayostahili.
Alisema kuwa barabara zilizojengwa ni barabara ya Ikengeza Nyang'oro yenye
kilometa 10 kwa gharama ya shilingi milioni 264,049,000 kwa kiwango cha changarawe,matengenezo
makubwa ya barabara ya Ikengeza Igodikafu iliyogharimu kiasi cha 396,279,000.
Eng Jabiry aliongeza kuwa wamefanikiwa kufanya matengenezo ya barabara ya
Malizanga kilimeta 2,matalawe kilimeta 2,Mapogoro Kitisi kilometa 4.25 Makombe
kilometa 2,Kitanewa kilometa 5, pamoja na ujenzi wa Daraja mfuto barabara ya
Wasa Mahuninga ampo zimetumia kiasi cha shilingi milioni 279,638,700.
Aidha ENG Jabiry alisema kuwa wanaendelea na ujenzi wa dharura wa daraja
la TAO katika barabara ya Kitayawa na Lupembelwasenga ambalo lilisombwa na maji
kutoka na kunyesha kwa mvua nyingi za masika na daraja hilo litagharimu kiasi
cha shilingi milioni 123,265,000.
Alisema kuwa katika wilaya ya Iringa wamefanya matengenezo na ujenzi wa
barabara ya Kibena Mfukulembe yenye kilometa 5.06,matengenezo ya kawaida ya
barabara ya Ilandutwa Ifunda kilimeta 3,Udumka Igomtwa kilimeta 2 kwa gharama
ya shilingi milioni 110,085,000 na matengenezo maalum ya barabara ya Ifunda
Bandabichi Itengulinyi kwa gharama ya shilingi yalingi milioni 984,238,710.
Eng Jabiry alimazia kwa kusema kuwa kukamilika kwa barabara hizo kutachochea
maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi kutoka na kurahisishiwa usafiri na
serikali.
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga aliwataka Wakala wa Barabara
za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawashirikisha
viongozi wa maeneo husika wakatia wa ujenzi na ukarabati wa barabara hizo.
Sendiga alisema kuwa wananchi wamekuwa wanaharibu miundombinu ya barabara
kutokana na kutokuwa na elimu ya umuhimu wa barabara hizo hivyo ni muhimu kwa
TARURA kutoa elimu kwa wanachi jinsi ya kuzitunza barabara hizo.
Alisema kuwa ni muhimu kuendelea kuwasimamia wakandarasi ili wamalize kazi kwa
wakati unaotakiwa na ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo
imetolewa na serikali.
Lakini Sendiga aliwaagiza viongozi wa TARURA kuhakikisha kila barabara
inayojengwa inakuwa na mitaro ambayo itapitisha maji ili kuzilinda barabara
zisiaharibike mapema.
Sendiga alisema kuwa anawapongeza TARURA wilaya ya Iringa kwa kazi kubwa
wanayoifanya ya kusimamia wakarandarasi kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa
kulingana na thamani ya fedha husika
Post A Comment: