Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa, amewataka wafanyabiashara  wote kwenye eneo lake kuweka walinzi kutoka kampuni zinazotambuliwa na serikali ili kuepuka udanganyifu

Ameyasema hayo leo April 20,2023 kwenye  kikao cha pamoja na wafanyabiashara wa Mtaa wa Dome kilicholenga kuweka mikakati ya kuzuia mianya ya wizi,hasa kwenye maduka na maeneo mengine ya Biashara.

Mwenyekiti huyo amesisitiza wafanyabiashara wa Mtaa huo kuweka walinzi kwa  mikataba inayotambuliwa kupitia uongozi wa serikali ya Mtaa ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

“Chukueni kampuni za ulinzi ambazo zinafahamika kisheria na ule mkataba muusome na muuelewe na kuma mikataba mingine siyo mizuri niwaombe wafanyabiashara kama kuna watu wanahitaji kuingia mkataba na walinzi ofisi ya serikali ya mtaa ni mdhamini wa moja kwa moja kwenye mikata hiyo tatizo likitokea kwako wewe unakuja moja kwa moja ofisini ukitoka hapa tunawasiliana na kata ukitoka kwenye kata tunawasiliana na mkuu wa kituo ukitoka kwa mkuu wa kituo tunawasiliana na kamanda wa jeshi la polisi Mkoa”

“Tunahitaji tuitunze mitaji yetu usihangaike na mtu ambaye hataki kuchangia fedha ya ulinzi wewe leta taarifa ofisini hapa sisi tutamshughulikia ikiwa ni pamoja na kutumisha kwenye mtaa wa kwetu bora ikajulikana eneo furani mpo watatu lakini biashara yetu iko salama kila siku mlizi yupo na mnakuta mali zetu ziko sawa”.amesema Mwenyekiti wa mtaa Najulwa

Baadhi ya wafanyabiashara zaidi ya watano (5) wakazi wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, wamelalamikia hali ya kukithiri kwa wizi kwenye maduka yao ndani ya wezi mmoja.

Wameeleza kubomolewa magufuli ya kwenye milango ya biashara yao na kuibiwa vitu na mali mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara ikiwemo Mchele, Maharage, Simu, Tv, Vocha, gunia la viazi, Mafuta, Sukari, pamoja na fedha.

Kwa upande wake polisi wa kata ya Ndembezi Jastin Nyatano amesisitiza suala la wananchi kuchukua hatua za kuimarisha ulinzi na usalama wa mali zao kwa kushirikiana na jeshi hilo.

Nyatano amewasihi kuchukua tahadhari juu ya watu wanaoendelea kutapeli kwa kuchukua fedha, mali na vitu mbalimbalimbali kwa lengo la kulinda mali zao.

Aidha Nyatano amewaomba wafanyabiashara hao kutoa taarifa za vitendo vya ukatili unaoendelea kufanyika katika maeneo yao ya biashara kwenye jamii na sehemu zingine ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Kikao hicho ulioandaliwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ulilenga kuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao,ikiwemo maeneo ya Biashara.

Inasadikika wezi hao siyo wakazi wa mtaa wa Dombe na kwamba baadhi ya wakazi wa Dome kushirikiana na wezi hao katika hatua za kutambua maeneo ya wafanyabiashara na hadi kufikia hatua ya kuvunja Magufuli ya milango yao.

 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa akiwasisitiza wafanyabiashara wa mtaa huo kuweka walinzi kwenye biashara zao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa akiwasisitiza wafanyabiashara wa mtaa huo kuweka walinzi kwenye biashara zao.

Polisi wa kata ya Ndembezi Jastin Nyatano akiwasii wafanyabiashara hao kuimarisha ulinzi na usalama wa mali zao


Kikao kikiendelea katika eneo la ofisi ya serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambacho kimefanyika leo Alhamis April 20,2023.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: