Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo Mohamed Hassan Moyo akimsomea makosa yake mwenyekiti wa Kijiji cha Naipingo Christopher Ngunyali wa mwisho kulia aliyevaa kofia nyeusi mbele ya wananchi wa Kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naipingo Christopher Ngunyali akijibu tuhuma zinazomkabili mbele ya mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo kabla ya kuamua kujiuzulu cheo hicho cha uenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Naipingo



Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MWENYEKITI wa serikali ya Kijiji cha Naipingo kata ya Naipingo wilaya ya Nachingwea Christopher Ngunyali amejiuzulu madaraka yake baada ya kukutwa na tuhuma mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho.

Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo, mwenyekiti huyo Christopher Ngunyali alisema kuwa anajiuzulu cheo hicho kutokana na kukutwa na tuhuma za kutokuwa na uhusiano mzuri na wananchi.

Ngunyali alikiri mbele ya mkuu wa wilaya tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa mmoja ya wananchi kutokana na majibizano waliyokuwa wanajibizana na mwananchi huyo hadi kupeleka kumtolea lugha za matusi.

Lakini pia Ngunyali alizikana baadhi ya tuhuma zikizokuwa zinamkabiri mbele ya mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ambazo ni kutolipa faini ya kutoa lugha ya matusi kwa mwananchi,kufanya kazi kwa mabavu na Kuingilia majukumu kamati nyingine za serikali ya Kijiji.


Ngunyali alisema kuwa alichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwaongoza wananchi wa Kijiji cha Naipingo lakini kutokana na kwenda tofauti na mtendaji na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi CCM tawi la Naipingo ndio kumepelekea kutungiwa hizo tuhuma hivyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Kijiji hicho ameamua kujiuzulu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa anabariki maamuzi yaliyochukuliwa na mwenyekiti huyo Christopher Ngunyali kuamua kuachia madaraka kutokana na tuhuma mbalimbali zikizokuwa zinamkabili.

Moyo alisema kuwa mmoja ya wenyeviti wa vitongoji wa kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa Kijiji cha Naipingo hadi pale uchaguzi utakapoitishwa na tume ya uchaguzi.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kaimu mwenyekiti wa Kijiji hicho kwa kufanya shughuli za kimaendeleo hadi pale watakapo mwenyekiti mpya.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: