Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Njombe imeandaa kampeni maalumu ya Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ambayo itaitwa na Simama na Mama kufuatia Utekelezaji mbalimbali wa Miradi inayoendelea hapa Nchini ambayo imetekelezwa kwa Muda Mfupi Tangu alipoingia Madarakani.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe kupitia Jumuiya ya Vijana Samweli Mgaya amesema kuwa Kampeni Hiyo yenye Maudhuio ya Kueleza mambo yote yaliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita ambapo Wataandaa matamasha na midaharo mbalimbali ili kueleza kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya Rais Sami Suluhu Hassan.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo amesema kuwa anaamini Uungwaji Mkono wa kampeni hiyo na makundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Njombe na Nje ya Mkoa utasaidia kuondoa Propaganda chafu zilizokuwa na lengo la Kumchafua Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzani.

Pia ameeleza kuwa kampeni hiyo itakuwa Mkoa wa Mzima wa Njombe na Hivyo Vijana Watelezwa fursa mbalimbali zinazotolewa bna Serikali Ikiwemo namana ya Kupata Mikopo ya Asilimia 10 Kwa Wanawake na Vijana kutpoka katika Halnmashauri zao.

Kwa Upande Wake katibu wa Jumuiya Hiyo Khamis Kachinga amesema kuwa Jumuiya Hiyo itahakikisha inasimamia na Kufuatilia Mienendo ya Watumishi wa Serikali ambapo sio waaminifu ili wachukuliwe hatua stahiki kilingana na makosa yao kwani kufanya ubadhirifu wa aina yeyote ni kumrudisha Nyuma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani katika kuwatumikia Watanzania.

Kampeni Hii inatajwa kuwa itawahusisha Wadau mbalimbali wa Chama Na Serikali pamoja na Asasi za Kirai na Viongozi Wa Dini.
Share To:

Post A Comment: