Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Askofu mteule Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu leo amewekwa wakfu kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Victoria.

Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu huyo  Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu na msaidizi wa Askofu mteule Mch. Daniel Henay Mono imefanyika  katika kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga  ambapo  ibada hiyo imeongozwa na  mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo.

Akiongoza ibada hiyo Askofu Dkt. Fredrick Shoo amemweka wakfu na kumtangaza  Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Victoria.

‘Natangaza mbele ya umati huu wa mashahidi kuwa leo kuanzia siku hii ya Bwana ya tatu baada ya Pasaka tarehe ya 30 ya Mwezi Aprili Mwaka huu 2023 wewe Mchungaji Dkt. Yohana Ernest Nzelu umekuwa Askofu wa Kanisa la Mungu katika jina la Baba nala Mwana nala Roho mtakatifu nenda sasa ukatumike kama Bwana alivyopenda kukutumia Amina’

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu huyo ameahidi kutoa ushirikiano katika huduma za Dini pamoja na hudumza kijamii na kwamba amewapongeza viongozi wa serikali kwa ushirikiano wao na viongozi wa Dini huku akiwaomba kuendelea kushirikiana siku zote.

Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu wakati akizungumza kwenye ibada hiyo ametaja  baadhi ya changamoto zinazokwamisha huduma za Kanisa pamoja na changamoto za wananchi hasa katika Mkoa wa Shinyanga.

‘Bado kunauhitaji mkubwa wa barabara za mitaa katika Wilaya ya Kahama na pia kumalizia kipande cha Old Shinyanga hadi Bubiki, kuna changamoto juu ya ujenzi wa ukarabati wa uwanja wa Ndege wakazi wa mikoa hii miwili Shinyanga na Simiyu wanapata adha kubwa sana ya kuunganishwa na maeneo mengine kwa njia ya anga ombi langu kwa serikali kwa mara nyingine tene iangalie mchakato huu uweze kukamilika’

‘Tunatiwa moyo sana na miradi ya kimkakati inavyoshughulikia tunaona kazi zinaendelea na tunaona kazi za bomba la mafuta tunaomba sana ajira zizingatiwa wazawa wenye ujunzi wa eneo husika’

‘Kuna umakini unahitajika sana kwetu sote hasa juu ya kukaribisha asasi zisizo za kiserikali kwa habari tunazoziona mitaani na kuzisikia hili swala la ushoga ni janga linalotakiwa kupigwa vita sana katika Nchi yetu hili ni chukizo mbele za Mungu   tunatamani kusikia sauti kali ya serikali dhidi ya jambo hili sisi kama Kanisa kwa nafasi yetu tunaahidi kutoa ushirikiano katika kupigana vita hii na Mungu atusaidie’

Akitoa salam za serikali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme amesema serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa Dini na  kushughulikia changamoto zilizopo katika Mkoa wa Shinyanga

‘Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za  Dini ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu, katika changamoto zilizotajwa ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara Wilaya ya Kahama napenda kuwataarifu kuwa serikali imeanzisha mradi unaojulikana kama Taktiki ambao unalenga kuboresha miundombinu miji 45 za Tanzania zikiwemo Manispaa zetu mbili za Wilaya ya Kahama na Shinyanga mjini kupitia mradi huu Manispaa ya Kahama itajenga kil. 24. 2 kwa kiwango cha lami lakini pia itajenga stendi kuu ya mabasi cha kisasa na soko kuu la kisasa’

‘Ujenzi wa kiwanja cha Ndege katika eneo la Ibadakuli Shinyanga napenda kuwataarifu kuwa utekelezaji wa ujenzi umeanza kwa Ghalama ya Shilingi Bilioni 52 na Milioni 868 Mheshimiwa Rais tayari amekwisha zitoa fedha hizi mkandarasi tayari amekabidhiwa eneo la mradi na utekelezaji wake unakamilika ndani ya Miezi mitatu, changamoto zingine za ujenzi na ukarabati wa barabara Mkoa wa Shinyanga  tayari serikali yetu imeanza kuzifanyia kazi’

RC Mndeme amewakumbusha wakristo kuzingatia misingi ya Dini huku akiwasihi viongozi wa Dini kushirikiana ili kutokomeza mmomonyoko wa maadili katika jamii na Taifa kwa ujumla.

‘Tuendelee kuheshimu imani yetu pia wazazi na wananchi tuendelee kuwalinda watoto wetu dhidi ya ukatili wanaofanyiwa tukemee matendo yasiyofaa kwa vitendo tuziishi amri 10 tulizopewa na mwenyezi Mungu na sisi serikali hatuyabariki mambo yanayoenda kinyume na tamaduni zetu viongozi wa Dini, serikali na jamii nzima tuungane kwa pamoja kusimamia maadili ya watoto wetu, amesema RC Mhe. Mndeme

Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu leo Jumapili Arili 30, 2023 amewekwa wakfu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Victoria ambapo ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na serikali huku mgeni rasmi akiwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo akizungumza kwenye ibada ya kuwekwa wakfu Askofu mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu na msaidizi wake Mch. Daniel Mono katika Kanisa kuu la Ebenezer mjini Shinyanga.

Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu wa kanisa kuu Ebenezer akizungumza baada ya kuwekwa wakfu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.. Christina Mndeme akitoa salam za serikali kwenye ibada hiyo.

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 








Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.

Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.

Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: